CHOMEZO MALKIA WA JELA SEHEMU YA TANO
SEHEMU YA TANO
.............................. ...
Baada ya kupambazuka NYANZARA aliamua kumpatia adhabu ya kufyeka nyasi kwa kumpangia eneo kubwa na kutaka wakat wa chakula utakapo fika asionekane LINDA akiwa anaendelea na adhabu aliyopewa alikuja afande MUGA na kuweza kuongea na NYANZARA ndipo NYANZARA akaonekana kumwita LINDA ,LINDA aliacha fyekeo na kwenda kumsikiliza "Afande anakuita kaongee nae hakikisha hii kazi unaimaliza ukileta ubishi utakufa njaa " aliongea NYANZARA ,LINDA alimfuata Askar MUGA mpk ofisin kwake "LINDA pole Sana "aliongea Askar LINDA hakumjibu chochote kile "Usiwe mkimya ongea na Mimi nikusaidie "
"Afande Mimi siwez naogopa "
"Hakuna cha kuogopa hakuna atakae jua na haswaaa nitakuwa nikikuiba nyakat za usiku wanapokuwa wamelala wenzio na kwenda kufurah nje ya gereza pamoja au unapenda kuteseka hiv unavyo teseka " Maneno ya afande MUGA yakaanza kumwingia taratibu "Lakin NYANZARA anavonifanyia siyo vizur Chakula cha Leo sintokipata ndo adhabu yangu pamoja na kufyeka eneo lile lote kubwa ulilonikuta "
"Usijali nenda kaniitie afu mm ntaonana nawewe Usiku " LINDA alitoka na kwenda kumwita NYANZARA Kuna kitu ambacho aliambiwa na afande akaonekana akiwa amechukia na kwenda kumwambia LINDA aweze kuachana na ile kazi na kurud ndan ya gereza
Ilipofika majira ya usiku wafungwa wote wakiwa wamelala Afande MUGA hakuweza kwenda nyumban kwake mpk atakapoona na LINDA aliweza kuongea na askar aliyekuepo lindo sehemu ile ya gereza na kuweza kumpatia chochote kitu ili aweze kuonana na LINDA yule askar alifungua get na kwenda kumwamsha LINDA na kutoka nae nje afande MUGA aliweza kusogea nae kwa pemben hili waweze kuongea "Ulikuwa umelala ?" Aliuliza afande "Ndiyo niliona umechelewa Sana nanilikuwa na usingizi "alijibu LINDA huku akipikicha macho yake kwa mikono na kupiga mihayo "Sawa sasa nisikilize nahitaj jibu langu la swali nililokuuliza asubuh uko tiyar ama ?
LINDA alikuwa akiangalia huku na huku huku akikuna kichwa chake kutafuta jibu "Niambie " aliongea afande MUGA "Nimekubali "
"Safi Sana huto jutia nakuapia Utafurahia kuwa namm utaona ulichelewa " alisema afande MUGA na kumsogelea kwa karibu LINDA huku akijaribu kupeleka midomo yake katika shavu la LINDA ,LINDA aliwah kumzuia "Nini sasa ? Aliuliza afande "Unataka kufanya nn Tutaonekana we huon kuna maaskar wanazunguka niache nikalale jibu lako nimeshakupa "
"Haya we nenda kalale nitakuona kesho sasa naweza kurud nyumban nikiwa na furaha "Aliongea fiance MUGA na kuweza kumrudisha LINDA ndani
Baada ya kupambazuka nje ya eneo la mahakama nyumban kwao na LINDA anaonekana mama yake mdogo na LINDA akiingia ndani Mama yake LINDA alipomwona mdogo wake alimtaka aondoke "Dada mim naomba unisamehe sikujua Kama yatakuwa haya ningelijua hata nisingelifanya "
"Amanda wewe ni mtu mbaya Sana sidhan Kama kweli wew ni ndugu yangu wa damu kwel wa kufanya hivi na kwann hukunishirikisha unajichukilia tu maamuz " aliongea mama yake LINDA huku akionekana kuwa na hasira "Dada punguza hasira nimekosa nimejua sawa nakuomba msamaha siku zote hiz je nisingekwambia hilo jambo ungejua "
Sasa Kama huku taka nijue kwann ulinambia najua umefurah kuona mwanangu anaozea jela umefanikiwa "
"Mim naomba tuyamalize tu nilifanya hiv kukusaidia kumbuka ulitaka BEN asiendee kuwa na mwanao nikaona bora nimtafute yule binti ila sikuwa najua Kama yangetokea haya "
"Amanda usijitetee mim sinto kusamehe mpk nakufa mtoto Ana uma "
"Lakin mim ni ndugu yako kumbuka "
"Mmh potea mbali naomba utokee kwangu " Mama LINDA alimsukuma na kumtoa mdogo wake njee na kufunga mlango wake alirud na kukaa kwenye kochi huku machozi yakimtoka
Baada ya siku kadhaa kupita Amanda aliamua kwenda alipokuwa anakaa TABU lakin hakuweza kumkuta kwa kuwa alikuwa kaisha hama baada ya lile tukio kutokea aliamua kumtafuta mtu wa karbu na TABU na kuweza kuelekezwa alipoamia Hakutaka kuchelewa alimua moja kwa moja kwenda mpk nyumba aliyoelekezwa baada ya kufika na kubisha hodi TABU akiwa seburen ameweka Headphone masikion akisikiliza mizik aliweza kusikia hod kwa mbali aliitoa aweze kuhakikisha alipoona n kwake alinyanyuka na kusogea kufungua mlango na kukuta ni Amanda TABU alishtuka na kutaka kuwah kurudishia mlango Amanda aliusukuma na kuweza kuingia ndani "Unafunga nn sasa unadhan nisinge pajua ulipoamia" aliongea AMANDA "Lakin sikuja kukudai pesa ulizo niahid utanipatia "Aliongea TABU "Kwasababu ulijua ulilolifanya "
"Amanda ulinipa kaz niliamua kufanya vile kwaajili yako uliniomba mim na mpenz wangu pia unadhan angejua hili ingekuaje "
"Anhaaa ko wewe uloyafanya n mazur "
"Mim nilifanya Kama ulivotaka nifanye "
"Nilikwambia uende nyumban kwake "
"Amanda hayo yashapita bwana Kama Una dili jingine nambie ila Kama umekuja na Yale Yale naomba tu ungefanya uende "
"TABU naondoka labda na hapa uame nitarud "
"Bwana Eeeh! Sikukulazimisha unitafute tusitishane sijala hata shiling tano yako usinisumbue na hapa wala sinto hama nihame kwaajil yako Ina husu " AMANDA alimtazama kwa hasira na kuamua kuondoka "Mxxxxxxiiiiu watu wengine Hela yenyewe hajanlipa kunisumbua tu" alirud kukaa na kurudisha headphone masikion kwake
Katika maeneo ya gerezan NYANZARA alivuliwa uongoz na kukabidhiwa msichana LINDA aweze kuongoza LINDA aliamua kutoa woga wake wote kwakua alikuwa tayar kapata uongoz na NYANZARA Kuwa chin yake Siku mbili baadae Afande MUGA alimwita LINDA ofisin kwake waweze kuongea "Unajisikiaje sasa ?" Aliuliza Afande "Nafuraha kupita kias sikujua Kama ni raha kias hiki "
"Nilijua utakuwa mpole kumbe na wewe humo Eeh"
"Unajua unapopata nafas itumie acha niitumie "
"Hii inakufaa tena haswaaa na ulivo mzuri hukufaa hata kidogo kuteseka wewe ni MALKIA "
"Hahahahaa Afande inamaana mm ni mzur kias hiko "
"Ndiyo we unadhan kwann nimekuchagua wewe kwan hao wengine sikuwaona waliofika kabla yako "
"Haya Bhana ahsante "
Majira ya usiku LINDA akiwa na PENDO ,PENDO alitaka kujua kuna nn kinaendelea "LINDA kuna kitu ambacho unanificha haiwezekan wewe hauna hata muda mrefu tangu umeingia halafu Leo hii wewe ni NYAMPAL A" aliuliza PENDO "Mh! Kwahyo labda wewe unahis kuna kitu gani ?
"Mimi sijui ila ndo nataka kujua wewe n rafiki yangu usinifiche niweke waz nijue "
"PENDO hakuna chochote kile wameamua kwasababu wameona ninafaa kuwa "
"mmmh Haya "
Siku iliyofuata wafungwa wote wakiwa wanafyeka nyasi NYANZARA alikuwa amekaa chini ya mti hafany chochote kile LINDA alipomwuona alimfuata na kumpa fyekeo "wewe usijifanye huon wenzio wanachokifanya ufanye kunyanyuka hapo ukafanye kaz" aliongea LINDA "Sifanyi lolote naomba uniachee "
"Utanyanyuka unyanyuki "
"Nimeshasema sifanyi "
LINDA aliondoka na kwenda kumfuata afande MUGA ,Afande MUGA alikwenda na kumwamrisha NYANZARA aweze kufanya anacho amrishwa na kiongozi wake Baada ya afande kuondoka NYANZARA alinyanyuka kwa hasira na kuanza kupigana na LINDA wafungwa wenzao waliacha kifanya kaz na kusogea kushangalia ugomvi ule ndipo maaskar waliokuepo karibu walisogea na kuwaamua afande MUGA aliamua kumpa adhabu NYANZARA kwa kumpatia eneo kubwa ambalo atakiwa akifanya usafi kila siku mpk atakapo limaliza lote huku akisimamiwa na LINDA pamoja na askar mmoja ambaye alikuwa akiwasimamia tangu mwanzon kumsimamia aweze kuifanya adhabu ile kadri ya siku zilivo zid kwenda na LINDA kuzoea uongoz wake alikuwa akiwapelekesha Sana wafungwa wenzie na wengine kutokea kumchukia ila hakuonekana kujali hilo kwa kuwa alikuwa tayar ana mtu ambaye anamtegemea Sana ila rafiki yake PENDO alikuwa akijarbu Sana kuomwomba LINDA aweze kubadilika Tabia yake na kuweza kukaa vizur na wenzake ila ilo lilikuwa n gumu Sana kwa LINDA
No comments