Kujamiiana na Roboti Kutasababisha Kupungua Kwa Tendo Hilo Baina ya Binadamu Kufikia Mwaka 2050


Kushiriki ngono na mashine au roboti kunaweza kufanya binadamu wapunguze kufanya tendo hilo wao kwa wao ifikapo mwaka 2050, wanasayansi wameonya.

Mtaalam mmoja wa roboti amedai kuwa mapenzi na roboti yanaweza kuwa na uraibu na siku za mbele zaidi kupoteza kabisa ushiriki wa tendo hilo baina ya binadamu kwa binadamu.

Kama teknolojia zingine ambazo zimechukua kazi za binadamu, roboti wanaweza kupita uwezo wa wanaume, na kuwa wapenzi bora.

Akizungumza na Daily Star, Joel Snell, mtaalam wa roboti kutoka chuo cha Kirkwood cha Iowa, alisema: ‘ Mapenzi na roboti yanaweza kutengeneza uraibu. Roboti wa ngono watakuwa wakiwepo daima na hawawezi kusema hapana.’

Pamoja na kupatikana muda wote kwaajili ya tendo hilo, roboti wanaweza kuwa wajuzi zaidi katika mapenzi kuliko binadamu.

Snell aliongeza: Kwa sababu watakuwa wametengeneza utaratibu mahsusi, roboti wa ngono watakidhi kila hitaji la mtumiaji.

No comments