Mambo yatakayokusaidia kudumu katika mahusiano ya kimapenzi




Kuna wakati ifike pahala watu waweze kutulia katika mahusiano yao ya ndoa, ila jambo hili linakuwa gumu kwa sababu watu hao wamekuwa hawafahamu mambo ya msingi yatakoyowasidia waweze kudumu katika mahusiaano kwa muda mrefu.

Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.

Hivyo ili penzi liweze kuwa bora Zaidi kila wakati inatakiwa wapenzi hao waweze kufanya mambo yafutayo ili kupalilia penzi hilo.

kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi pia.

Zungumzeni hisia zenu kwa pamoja
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

No comments