Njia Nne Za Kufanya Ili Uongeze Kujiamini Kwako kwa Wanawake
Kuweza kujiamini kwa mwamume ni jambo muhimu katika huu ulimwengu ambapo kunatofautisha kati ya mwanamume thabiti na wale feki. Kila mwanamume anajaribu kuimarisha kujiamini kwake katika huu ulimwengu. Lakini ushawahi kujiuliza ni mbinu gani unazofaa kutumia ili uongeze ama kuimarisha kujiamini kwako? Wengi wasiojua mbinu za kutumia kuwa na confidence wanabakiwa na kutumia mbinu ambazo mwishowe zinawaweka katika hali ambayo inakuwa aibu kwao.
Tukiongea kuhusu maswala ya kujiamini, wanaume wengi kujiamini kwao mara nyingi hutumika wakati ambapo anajaribu kumtongoza mwanamke fulani ama wakati ambapo anajaribu kumridhisha mpenzi wake ili azidi kumpenda zaidi na zaidi.
Well, kwa wanaume, kuna wale ambao wanajiamini na kuna wale ambao bado kujiamini ama kuwa na confidence kwa mwanamke ni tatizo.Labda kuna mwanamke ambaye ushawahi kujaribu kumtongoza halafu baada ya siku ama madakila ya kuongea naye anakupuuza ama anakudhalilisha mbele ya marafiki zako. Usikate tamaa kwani bado una nafasi kubwa ya kujua kosa lako limetokea na wapi.
1. Jikumbushe kuwa wewe ndiwe wewe
Wanaume wengi wanafanya makosa makuu ya kujidhalilisha kibinafsi. Hii inatokea pale ambapo mwanamume anapomakinika na mambo ambayo yanamfanya yeye duni. Maneno ya kujiona kama wewe hufai ama kujiona kuwa mwanamke unayemfukizia hatapendezwa na tabia zako unafaa kuyatupilia mbali. Unafaa kumakinika na mambo ambayo yana uzuri kwako. Mfano kujiamini ya kuwa una kipawa cha kuongea, kuchekesha nk. Kujiamini huku kutamfanya mwanamke kukudhanimi. So kazi ni kwako, aidha usijiamini mwanamke akudharau ama ujiamini wanawake wakuandame kama vile kivuli.
2. Usimakinike sana na urembo
Kosa jingine ambalo wanaume wengi wanafanya ni kuwa wanamakinika sana na urembo wa mwanamke. Ukweli usemwe, ukiwa umezungukwa na wanawake wengi warembo kwa kawaida inakuwa vigumu kumakinika na yale ambayo unasema. Hii hutokea kwa sababu ya kufikiria sana urembo wa mwanamke kiasi ya kuwa unapunguza kujiamini kwako. Kusuluhisha hili tatizo hakikisha ya kwamba wakati ambapo unapokuwa na mwanamke mrembo yeyote, weka kwa akili yako kuwa mwanamke huyu ni mbovu na hana lolote na urembo, hii itakupa wewe uwezo wa kumwona mwanamke unayeongea naye ni wa kawaida hivyo kukupatia nafasi rahisi ya kuongea naye bila tatizo.
3. Shughulika na maswala mbadala
Wakati mwingi ambapo mwanamume anapokuwa date na mpenzi wake ama kukutana na mwanamke kwa mara ya kwanza, kitu ambacho anakiweka mbele ni malengo na madhumuni ya kutaka kitu kutoka kwa mwanamke. Aidha inawezakuwa anataka namba ya simu, kupewa date nyingine ama kitu tofauti mbali na haya.
Ok mbona usimakinike utulie uje na mtindo mpya ambao utakufanya uwe na confidence kwa mwanamke yeyote? Jaribu kuleta maswala ambayo hayalengi ajenda yako kwa mwanamke ili uweze kupata confidence. Njia hii inapunguza wasiwasi wako ambao unaweza kuwa nao kwa mwanamke yeyote. Mwishowe wakati umemzoea itakuwa rahisi kwako kuweza kumwambia chochote ambacho umekuwa ukitaka kumwambia.
4. Rudiarudia
Wataalamu wengine wangepinga mbinu hii ya kutumia kwa mwanamke wakati wa maongezi lakini kwa mtizamo flani hii ni njia muruwa ya kutumia wakati wa kujenga kujiamini kwako kwa mwanamke. Kama una mistari ambayo umeishika na kwa kawaida unaitumia wakati unapokuwa na mwanamke na umeshuhudia kuwa inafanya kazi kila wakati, mbona usiitumie tena na tena kwa mwanamke unayemzimia kwa sasa? Hii kando na kukupatia confidence, itakupa nafasi ya kuonekana mtulivu na kukuona kama unajua kupanga maneno yake vile inavyotakikana.
Kujifunza kujenga kujiamini kwako kando na kuwa kutakuwezesha kuweza kuongea na wanawake kwa urahisi, pia kutakuwezesha wewe mbeleni kuweza kukabiliana na mambo kadhaa na kufanikiwa maishani.
No comments