Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi
Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi
KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI..!
zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA..
👉VIGEZO VISIVYO NA MSINGI.
🔹Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe.
🔹Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi kama hayo.
🔹Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi.
🔹kuna msemo usemao, "ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu" na mwingine ufananao na huo unaosema "mchagua nazi hupata koloma".
👉NAMNA UNAVYOJIWEKA.
🔹Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.
🔹Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.
🔹Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasua? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.
🔹Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.
🔹Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.
👉MANENO UNAYOJITAMKIA.
🔹Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao.
🔹Utakuta Binti kwa sababu aliumizwa na kijana fulani basi, anasema Wanaume wote ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoji, mara Wanaume wote ni waongo, baba mmoja na mama mmoja.
🔹Sikia nikuambie, kinywa chako kina uwezo wa kuumba. Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.
🔹Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu(Mwanzo 1 :26) , Mungu aliumba dunia kwa kupitia Neno, kadhalika hata sisi tunao huo uwezo wa uumbaji kupitia vinywa vyetu (Mithali 18 :18 - 20).
🔹Kama Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume atakayekuja kwako akiwa muongo. Kama Unasema sina shida ya kuolewa basi miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako.
👉KUTOKUSHUKA.
🔹Utii ni tatizo kwa mabinti wengi sana wa sasa. Wengi hawakubali kushuka, hawataki Kuongozwa wanataka kujiongoza wenyewe.
🔹Kumtii mwanaume wanaona kama ni jambo la kizamani, wanaita mfumo dume hivyo wanataka kuishi katika mfumo Jike.
🔹Napenda kusema wasichana wengi vazi la Suruali limeathiri mpaka fikra zao, hata akili zao pia zimevaa Suruali.
🔹Binti Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye si msikivu (jike dume), kama hautaki Kuongozwa basi wewe ni mwanaume sasa unataka mwanaume wa nini?
🔹Biblia inaweka wazi kuwa mwanaume ndiye aliyeumbwa kwanza kabla ya mwanamke, mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume na si mwanaume kwa ajili ya mwanamke. Mwanzo 2 : 18, 21 - 25.
🔹Binti kaa kwenye nafasi yako. Jivike kiremba cha Hekima na Utii.
👉MAAGANO ULIYOWEKA HUKO NYUMA.
🔹Kama kuna mtu mliahidiana kuwa mtaona halafu kwa sababu zisizo na msingi ukamuacha, basi hii inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kukufungia baraka yako ya ndoa.
🔹Kama kuna mtu ana nung'unika kwa ajili yako, kama kuna mtu ana lia kwa ajili yako huu unaweza ukawa mwiba kwako usiifikie ndoa au ukaifikia lakini isiwe salama.
🔹Kama kuna watu ulishindwa kutimiza ahadi uliyowaahidi unatakiwa kutubu dhambi hiyo na kutengeneza nao kwa kuwaomba msamaha ili usiwe na vifungo vinavyokuzuia.
👉KUKOSA MSIMAMO.
🔹Mabinti wengi sasa hawana msimamo linapokuja swala la kujizuia kufanya mapenzi.
🔹Nimewafanyia counselling mabinti wengi na zaidi ya 80% kama si 90% wanalalamika kuumizwa na wapenzi wao. Ninapowauliza kama walishafanya sex karibu wote wanajibu NDIO.
🔹Kama mwanaume umeshampa mwili wako ni nini tena atakachokihitaji kutoka kwako? Kama ameshakula sebuleni kuna haja gani ya kuingia Jikoni?
🔹Ukivua Sketi yako kabla ya ndoa, usitegemee kuvaa gauni (shela) la ndoa.
👉ROHO CHAFU.
🔹Zipo roho chafu (mapepo) zinazoweza kumfunga mtu asioe /kuolewa. Kuna wengine wamefunga ndoa za kipepo na majini mahaba na kuota wanafanya mapenzi na wanaume wasiowafahamu.
🔹Pia zipo roho zinazofuatilia ukoo toka kizazi hadi kizazi wasiingie kwenye ndoa. Unakuta watoto wa familia fulani wote hawajaoa au kuolewa wamezaa wakiwa nyumbani au wakiolewa ndoa hazidumu.
🔹Hapa maombi yanahitajika kuepukana na roho hizo.
👉KUKOSA MAOMBI.
🔹Kwa mtu aliyeokoka maombi ni msingi wa Kila kitu. Kuingia kwenye ndoa ni haki yako Kama mwana wa Mungu lakini Kama sio muombaji unaweza ukashindwa kuipata haki hiyo.
🔹Kuwa umeokoka sio kwamba umemaliza kazi, bali ndio umeianza kazi, umetangaza mapambano.
🔹Ufalme wa Mungu wapatikana kwa NGUVU na wenye nguvu ndio watakao UTEKA (Mathayo 11 :12).
……………………….
HIZO NI BAADHI YA SABABU YA KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI.
JICHUNGUZE NI WAPI UNAKOSEA NA UFANYE UAMUZI WA KUBADILISHA KOSA HILO.
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake….
Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako. Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba. Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Hakunaga mke anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe.
Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana.
Ujeuri weka pembeni!
#ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao#
NOTE: Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu. Panapotakiwa hekima na akili zitumie!
Cku njema
No comments