Sentensi 3 Ambazo Zinaweza Kukufariji Katika Maisha Yako.
1 - “KILA JAMBO LINA WAKATI WAKE”
Wakati au muda ni kitu ambacho hakina mipaka. Hakuna jambo au kitu kisichokuwa na wakati wake na mwisho wake. Kwa maana kuwa, muda/time ndio suluhisho la mambo mengi. Kila jambo lina mwisho na wakati wake. Hata shida ulizo nazo zina kikomo chake ambacho zitaisha. Kila unapokuwa katika kipindi kigumu tambua kuwa kipindi hicho kitapita tu kwani kina mwisho wake. Lakini pia kumbuka kuwa hata unapokuwa katika kipindi cha raha, nacho kina mwisho wake. Hivyo ukiwa katika tafakari hizo katika shida na raha, ridhika na kila ulichonacho.
2 - “UNAWEZA KUWA NA FURAHA PALE UNAPOAMUA KUWA NA FURAHA, KWANI FURAHA NI MTAZAMO WA MTU NA SIO UHALISIA KAMILI”
Umeshawahi kujiuliza furaha maana yake ni nini? Inaweza ikawa na maana tofauti kwa watu tofauti mfano, wapo wanaoona furaha ni pesa, wengine huona furaha ni kutenda mema, wengine hutafsiri furaha ni raha, urembo au chochote ambacho wanaona kinawapa furaha. Lakini ukweli ni kuwa, furaha ni fikra. Unaweza kuwa na furaha pale unapoamua kuwa na furaha hata kama mazingira na hali iliyokuzunguka inakupa huzuni. Angalia katika maisha yako, shukuru kwa kila jambo na weka mtazamo chanya katika mawazo na fikra zako.
3 - “SHUKURU KWA KILA JAMBO”
Kila kitu kina faida na hasara yake. Badala ya kulaumu kila kitu katika maisha yako unaweza kuangalia katika upande mwingine. Mfano, badala ya kuumia na kupoteza muda katika kufikiria ni changamoto gani unazo katika maisha unaweza kubadilisha mtazamo wako na kuangaliza faida za changamoto katika maisha na kuacha kuwaza maumivu yake. Changamoto hutujenga katika maisha na bila changamoto huwezi kuendelea mbele.
Tuzidi kuchukuru kwa kila jambo katika maisha.
No comments