Unajua Afya ya ngozi yako huanzia ndani?
hello,
Natumaini sote tu wazima.
Leo tushirikishane kuhusu umuhimu wa kujali afya zetu ili tuwe warembo zaidi nje hasa kuwa na muonekano na ngozi zenye afya.
Wengi tumekuwa tukipaka vitu nje kutatua matatizo mbalimbali kwenye ngozi mara kwa mara, wengine matatizo haya yanatulia kwa muda kisha yanarudi.
1. Tabia ya kunywa Maji
Maji ni kinywaji chenye faida kiafya hasa katika kufanya mifumo ya miili yetu ifanye kazi sawasawa. Maji yanasaidia kuweka uwiano sawa wa maji na mafuta katika ngozi hivyo kwa kiasi kikubwa kuipa ngozi muonekano mzuri na kupunguza uwezekano wa kupata chunusi. Iwapo una umri mkubwa kunywa maji mengi(ya Kutosha) kunaweza kusaidia kupunguza muonekano wa ngozi kuzeeka (wrinkle) kwa kuwa seli za ngozi zinakuwa kama zimejaa( plumb) hivyo kuboresha muonekano wa nje.
Kunywa maji kama sehemu ya mtindo wa maisha kutafanya uendelee kupata faida zitokanazo na maji lakin ukiacha tu utagundua umejirudi kuwa na wrinkles zinazoonekana zaidi au chunusi zinarudi na kuwa na ngozi kavu.
2. Zingatia mmeng'enyo wa chakula unachokula
Kama tunavyojua, lishe ni kwa ajili ya kupata nguvu na kujenga/kuhuisha seli zetu ikiwemo za ngozi na hutokana na virutubisho mbalimbali tunavyokula, basi ni vyema tujali namna mwili unavyotumia virutubisho hivyo.
Kuna watu idadi fulani katika jamii(population) hupata matatizo katika kumeng'enya chakula aidha kutokana na matatizo katika mfumo waliozaliwa nao au kushindwa kumeng'enya aina fulani fulani za chakula hivyo kupelekea virutubisho katika chakula kutofyonzwa vizuri na kutumika na mwili au saa zingine chakula kukaa muda mrefu katika mfumo wa mmeng'enyo mpk kinachacha na kuzalisha bacteria wabaya mwilini.
Moja ya dalili za matatizo katika mmeng'enyo wa chakula ni pamoja na
-tumbo kujaa gesi
-kusikia kushiba sana(kuvimbiwa)
-tumbo kuwa kubwa kadri siku inavoenda wakati asubuhi unapoamka lilikuwa dogo kawaida
-kutopata choo vizuri, Kupata choo kidogo au baada ya muda mrefu mfano baada ya saa 48 kuendelea
Ukiona dalili kama hizi jaribu kukumbuka ulikula nini au ukila nini unapata moja ya hizi dalili, jaribu kukiacha uone kama kuna mabadiliko. Saa zingine hata ukiongeza kiasi cha maji ya kunywa unaweza kutatua tatizo na dalili hizo kupotea. Pia matumizi ya vyakula vyenye kambakamba(fibres) kama mboga mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa.
Mfano ukiona una tatizo kupata matunda au huwezi kula matunda ya sukari unaweza kuandaa kama kachumbari utakayotumia masaa ya asubuhi kama snack
weka Nyanya,kitunguu maji,pilipili hoho,karoti(sio lazima), tango, unaweza weka parachichi pia na unaweza kutafuna bamia mbichi pia.
ukila papai huweza kusaidia chakula kupita vizuri katika mfumo wa mmeng'enyo ukapata choo.
Chakula Kutomeng'enywa sawasawa hupelekea virutubisho muhimu kutotimiza malengo yake, mfano virutubisho ambavyo vilitakiwa kufika katika nywele au ngozi kupitia damu vinakuwa havifiki kwa usahihi.
3. Matumizi ya ngano na bidhaa zake
Hivi karibuni kumekuwa na uchunguzi kuhusu watu kupata mzio(alergy,inflamation) kutokana na matumizi ya ngano. Inasemekana ndani ya ngano iwe imekobolewa au laa kuna virutubisho ambavyo miili ya baadhi ya watu haiwezi kumeng'enya hivyo kupelekea hali ya mwili kushituka hasa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kupelekea dalili mbali mbali kama kusikia kichefuchefu sana, kukosa nguvu, sukari kupanda mwilini kwa muda mrefu n.k. Kisehemu hiki cha ngano kinafahamika kama Gluten, iwapo unasumbuliwa na vyakula vya ngano unaweza kupata matatizo katika kumeng'enya chakula hivyo kupoteza au mwili kutotumia vizuri virutubisho, kuongezeka sana uzito wakati unajiona kabisa huli sana ila unatumia ngano( mfano. oats) n.k.
4.Matumizi ya sukari
Kama tulivyoona kwamba maji yanabalance mifumo ya mwili basi sukari hufanya kinyume chake. Matumizi makubwa ya sukari huweza kupelekea ngozi yako kuonekana kama inazeeka, kuchoka kumbe yale maji unayokunywa yanakuwa kama hayatoshi kupunguza concerntration iliyopo. Kuna watu utasikia wanasema, "nikifululiza kunywa soda naota chunusi" kumbe hata mabadiliko ya diet (mpangilio wa kula) hupelekea kupata chunusi.
Ni vema tuzingatie kula mlo kamili, tupunguze milo ya fastafasta kama chipsi na tunywe maji ya kutosha ili tuwe warembo.
hugs
No comments