SHUGHULI YA NJEMBA ZENYE VIFUA VIPANA,NI HATARI KATIKA MAPENZI....!



Kuna mdahalo mkubwa ambao una majibu tofauti kuhusu wanaume wenye vifua vikubwa kama kweli wanapendwa sana na wanawake au la.
Unaweza ukakutana na mwanadada akimsifia mkaka kwamba anakifua kizuri akimaanisha kwamba ana kifua kipana ambacho kinajengwa kwa kufanya mazoezi maalum, aina hii ya mwanamke bila shaka inaonesha kuwa hupendelea zaidi wanaume wa aina hii na kwa hakika kama mume wake au boyfriend wake atakuwa na kakifua kadogo hatapenda sana na wala hataridhishwa na mwonekano wake kutokana na kupenda sana wanaume wenye vifua kabati (vifua vikubwa).
Matokeo yake ni kwamba ni rahisi zaidi kwa mwanamke huyu kushawishika na wanaume wenye mafua makubwa kwani wewe mwenye kidogo sio mapenzi yake.

Kwa upande mwingine usijeukashangazwa sana kukutana na mwanamke asiyetaka hata kusikia kuhusu hawa wanaume wenye vifua vikubwa na huhisi hata kichefuchefu kuona binadamu mwenye aina hii ya vifua. Hivyo kwa aina hii ya mwanamke hakika kifua kikubwa (six packs) sio dili wala mpango wowote na hata hawezi kushawishika na aina hii ya mwanaume,hivyo kwa mwanamke huyu mwanaume mwenye kifua cha kawaida ndio humzimia zaidi na huweza kuzuzuliwa kirahisi.

Hivyo basi kama mwanaume jambo la msingi ni kuangalia aina gani ya kifua mpenzi wako anapenda ndipo uamue kujenga kikubwa au kubaki hivyohivyo japo kwa asilimia kubwa kwa wanawake wa kisasa ambao wanataka waonekane kama wanakwenda na wakati hupendelea zaidi wanaume wenye vifua vikubwa kama vya wacheza mieleka.

No comments