KILA NIKIFANYA NAE MAPENZI- NAPATA MAUMIVU MAKALI SANA



Dada violet, pole na kazi, nahitji msaada wako kama utaweza kunisaidia nitakushukuru sana, pia kama inawezekana weka kwenye blog yako (ila usinitaje jina) ili niweze kupata ushauri zaidi,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, niko Zanzibar, tangu niwe mwali hadi leo nimekutana na wanaume wawili, mmoja aliniacha, kwa sababu ambazo hata sizielewi Mpaka leo hii na alinitamkia kabisa sina sababu ila tu sikutaki tena, iliniuma sana nilitamani hata kujiua, ukizingatia niliweka nadhiri kuwa atakaenibikiri ndie atakaenioa, lakini akawa ameshapotosha ndoto zangu,

Baada ya muda nikiwa chuo, nilipata boyfriend mwingine, ambae niko nae hadi sasa, cha ajabu kila ninapokutana nae, tukimaliza tu! Huwa naumwa sana hadi nameza dawa, yani akishaniambia kesho tutafanya mimi nitalala nawaza usiku kucha, Napata maumivu makali sana huku chini na maeneo ya kwenye kinena panauma sana, huwa naumia hata saa zima na jasho linanitoka kabisa

Huyu boyfriend wangu hadi anaogopa kunigusa, sasa nawasiwasi asije akashawishika kuwa na mwanamke mwingine, nampenda sana, na hata kwetu wameshamjua bado kuja rasmi tu!,

Aliwahi kunichukuwa kunipeleka hospitali moja huku huku Zanzibar, dada violet nilipimwa kila kitu, lakini hakukuwa na tatizo, hata daktari alishangaa, yani alichukuwa vipimo vyote, lakini hakukuwa na tatizo, siku ingine tena tulisafiri nae kwenda Kigoma, tulipofika tulilala pamoja hotelini, alivyonifanya tu! Sikulala hadi kunakucha, kiuno kinauma hadi miguu, asubuhi alinipeleka hospitali kule kule kigoma, napo wakaniambia kuwa sina shida

Tukakaa kama wiki mbili baada ya kutoka hsptl tukafanya tena, maumivu pale pale, nikaenda hospitali ingine tena kwa mara ya tatu, napo wakasema kuwa mimi sina tatizo lolote, wakampima hata na boyfriend wangu wakasema pia hana tatizo,

Hadi sasa sijielewi, maana nakosa kitendo cha muhumu kuliko vyote, naumia sana na hasa wasi wasi wangu ni kwamba huyu boyfriend wangu atanikimbia, Napata taabu sana naombeni mnisaidie nifanye nini? nawaza labda tatizo linaweza kuwa kwangu ndio maana hata mwanaume wa kwanza alinikimbia bila sababu

No comments