Madhara ya Kulawiti (Mapenzi Kinyume na maumbile)


VIJANA WAMEKOLEWA NA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
Madhara ya Kulawiti (Mapenzi Kinyume na maumbile)

Vijana wa siku hizi wengi sana hupenda kufanya kitendo hiki na kuona raha sana kuliko kutumia njia ya kawaida ambayo ndiyo njia sahihi, utakuta wakichukia sana pale wapenzi wao wanapokataa katakata kuingiliwa kinyume na maumbile. Hali hii hufanya wengi kwenda kuwahonga mashoga (wanaume waliojibadili jinsia zao) ili watimize haja zao.

Lakini umeshawahi kujiuliza ni kwanini vijana hupenda kufanya kitu ambacho jamii huchukia sana na hata mungu humlaani sana mtu anayefanya kitendo hiki. Au umeshawahi kujiuliza wale wanawake wanaopenda kufanyiwa hivi wanapata raha gani hasa na hali ya kuwa wananjia ambayo ni sahihi kutumia na je hawa wanawake unaifahamu hasa sababu yao wengi kufanya hivi? Ukweli ni kwamba nafsi ya mtu humpelekea kufanya kile kilicho kinyume na kisichopendeza hivyo ni juu yako kujiweka katika njia zilizo sahihi.

Wanawake wanaopenda kufanya hivi wengi hufanya kwa kulinda usichana wao usiharibike (Bikra) na utaona wakiingia ndani ya ndoa zao wakiwa bado ni wapya kabisa hata mume kuona raha kwa kuoa msichana mdogo (Bikra) lakini kuna siri kubwa sana huku nyuma ambayo aliificha huyu mwanadada ambayo ndio hii tunayoizungumzia. Hivyo wakiwa bado hawajaolewa hutumia njia ya nyuma kulinda heshima zao hapo baadaye. Na kuendelea kufanya hivi hujikuta wakiathirika kisaikolojia na kuona raha sana kutumia njia ya nyuma kuliko ya kawaida. Hii ni athari ambayo huweza kumkuta pale anapokuwa ndani ya ndoa kwani mume hatoweza kutumia njia ya nyuma na hivyo kukosa raha ya ndoa na kuamua kumtafuta au kuendelea na yule wa zamani aliyemzoesha uchafu huu.

Ni hali ngumu sana huwakuta pindi wanapotaka kujifungua kwani hukosa pumzi ya kumsukuma mtoto na hivyo kujikuta wakiwapa shida sana wakunga ambao wako tayari kumsaidia katika kuzaa kwake, na yule ambaye anajua makosa yake hujitahidi sana kuhakikisha anazaa kwa upasuaji ili aepuke aibu hii na kama ni mchezo wa mume na mke kufanya hivi basi wote wawili hufanya juhudi za kutaka kufanya upasuaji wakati wa kujifungua kuepuka aibu.

Wanaume wengi sasa hupenda kufanya hivi na kuona raha bila ya kujua kuwa wanapata madhara mbalimbali kama kisaikolojia na kiafya vilevile. Uaminifu ndani ya ndoa utapungua kwa kuzoea kufanya hivi kwni huwezi kumfanyia mkeo kitu hiki hivyo kwa kuhitaji kujiridhisha itakubidi umtafute wa nje ambaye atakubali kufanyiwa kitendo hicho.

Kama mmoja wa wafanyaji hawa wawili atakuwa na maambukizi basi ni rahisi sana kuambukizana maradhi kwani michubuko huwa ni rahisi sana kutokea kwa kufanya kitendo hiki cha kulawiti kwani sehemu za nyuma huwa na ngozi laini sana kulinganisha na njia ya kawaida. Na vilevile matatizo ya njia ya mkojo huweza kutokea kwa mwanaume anayefanya mchezo huu.

Vimelea vya maradhi huweza kusambaa kutoka sehemu ya nyuma kwa mwanamke mpaka sehemu ya mbele hasa kwa wale wanaotumia njia zote mbile kwa pamoja.

Mara nyingi tunapenda sana kuiga, hasa hasa vijana wa sasa hupenda kuangalia picha za ngono ambazo huwaathiri katika matamanio yao na kujikuta wakifanya kama kile walichokiona katika filamu za ngono. Fahamu ya kuwa wale wanafanya vile kwa maslahi ya kifedha na sio kwa matamanio, hivyo kuna njia nyingi za uongo wanazitumia kuhakikisha wanakushawishi ununue CD zao na hasa hutumia madawa fulani ambayo yanawafanya wafanye uchafu huo kwa muda mrefu sana hata zaidi ya nusu saa bila ya kufika kileleni, lakini sisi tukiangalia tunaona kawaida tu na kutaka kujaribu.

Fahamu ya kuwa njia ya nyuma ina kazi moja tu nayo ni kutoa haja kubwa ambayo ni uchafu, hivyo tusijilinganishe na wanyama hali ya kuwa tumepewa akili timamu za kujua kheri na shari hata hao wanyama wenyewe hawafanyi kitendo hiki sasa vipi tushindwe akili na wanyama? na tujitahidi sana kushauriana na kukatazana vitendo vinavyoweza kuharibu jamii yetu.

No comments