UNAIJUA RAHA YA KUFANYA NGONO?????



Raha ya mapenzi ni pale yanapofanyika kwa nafasi na usalama. Kila mmoja akaendelea kufurahia uhusiano kwa maana ameridhika katika njia ambayo ni salama kwa pande zote mbili.Ndugu zangu, penzi linanoga pale linapomhusisha mwanaume na mwanamke katika njia ambazo hazina madhara na si vinginevyo.

Ukitazama kichwa cha habari hapo juu, suala la watu kuingiliana kinyume na maumbile ni tatizo ambalo linaendelea kushamiri kwa kasi kama moto wa kifuu siku hadi siku katika kizazi cha sasa.
Linaonekana kuzoeleka na watu kutaka kulifanya la kawaida au kusema ndiyo fasheni ya kisasa. Kweli jamani!

Utasikia binti akikwambia kwamba bila kufanywa tendo hilo hajisikii raha. Anasema hivyo kwa sababu ya mazingira ambayo ameyapitia maishani, simlaumu kwa sababu tatizo hilo limehamia hadi kwa wanaume, kutokana na mazingira waliyoyapitia nao sasa wapo ambao hawasikii raha bila kufanya tendo hilo.

Utasikia mwanaume anakwambia bila kufanya kinyume na maumbile hasikii raha. Tatizo linakuwa hapo, anayependa kufanya mchezo huo akikutana na ambaye hapendi kufanya huwa unaibuka ugomvi na madhara yake inakuwa ni ugomvi kila kukicha.

Wanawake wengi wamekuwa wakinitumia ujumbe mfupi wakiniambia jinsi wanavyopata usumbufu kutoka kwa wanaume ambao wanapenda hako kamchezo.Wengi wamesema huwa wanakataa lakini wanaume huwa wabishi na wakati mwingine hufanya tendo hilo kwa kulazimisha au kujifanya wamekosea.

Historia inaonesha kizazi cha mababu zetu, mchezo huu haukuwa ukifanyika lakini vitendo hivi vimeshamiri kwa kizazi cha sasa kutokana na ujio wa DVD za ngono kutoka nchi za magharibi.
Watu wameona, wakakopi na kupesti katika uhalisia na kuona yanafaa. Wakaanza kuyatumia tena wakanogewa kiasi cha kusema: “Mimi bila kinyume na maumbile, sijainjoi mahaba.”

Taasisi moja ya Kimarekani imetoa taarifa kwamba licha ya magonjwa mengi ambayo yanaweza kusababishwa na tatizo la kuingiliana kinyume na maumbile lakini pia upo uwezekano wa mtu kuweza kuambukizwa kansa. Imeelezwa kuwa, virusi aina ya human papilloma ambavyo husababisha kansa huweza kuhama kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kupitia tendo hilo la kujamiana kinyume na maumbile.
Mbali na hilo, inaelezwa kwamba ni rahisi sana mtu kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi kutokana na msuguano unaosababishwa na ‘nature’ ya mazingira ya eneo husika ambalo halina majimaji ya asili yanayoweza kulainisha kuepusha msuguano ambao unaweza kusababisha magonjwa kusafiri kwa urahisi kupitia damu.

Nini kifanyike?
Licha ya kuwa wapo wataalamu wanaoshauri njia mbalimbali za kufanya ili kuhalalisha aina hii ya ngono iwe salama lakini nikushauri tu msomaji kuacha kabisa mchezo huu maana faida zake ni chache kuliko hasara.

Inatajwa kuwa huweza kuwasababishia wanawake matatizo wakati wa kujifungua kwa kutenda tendo ambalo linapingana na lile ambalo Mungu mwenyewe amelipitisha katika njia ya kuzaliana kupitia sehemu ya kawaida.

Hii ni tabia ambayo iliingia, tuna uwezo kabisa wa kuipinga kwa nguvu zote kwani raha ya mapenzi ipo katika mfumo mzuri ambao kila mmoja anaufahamu. Kwa yule ambaye ameshaathirika na mchezo huu, inampasa kubadilika na kurudi katika njia salama ambayo haina madhara mengi.

No comments