HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???
Jina mapenzi limeweza kupewa maana nyingi kulingana na maongezi yanayozunguka jina hilo. Mapenzi yaweza kusemwa kwamba ni jina linaloonyesha hisia za mtu iwe mahaba, pendo kwa mtu ama upendo wa Mungu.
Mara nyingi watu wengi hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba huhusisha ubongo wa mwanadamu.
Kuna aina nyingi za mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi.
Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo
Mapenzi ya kimwili (Eros)
Aina hii ya mapenzi ni ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi.
Hii ndio aina ambayo watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano.
Mapenzi ya Urafiki (Philia)
Aina hii ni ambayo inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako mzuri.
Mapenzi haya huwa sana ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule mwenzake.
Mapenzi ya aina hii yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa marafiki na dunia kwa jumla.
Mapenzi ya Familia(Storge)
Aina hii ya mapenzi ni inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao wanavyotegemeana.
Sifa za binafsi hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko huru na salama.
Mapenzi ya Kujitolea(Agape)
Aina hii ya mapenzi inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua. Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu.
Aina hii inahusishwa na kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile.
Dunia yastahili kuwa na aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni ni mfano mmoja wa kueleza aina hii.
Mapenzi Changamfu (Ludus)
Aina hii ya mapenzi ni mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza.
Aina hii ya mapenzi haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu.
Mapenzi Madhubuti(Pragma)
Aina hii ni mapenzi ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao wako katika ndoa.
Aina hii inahusishwa na uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka kudumu.
Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Kinyume na aina zingine za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia.
Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia)
Mapenzi haya ni ya mtu binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi, kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana kuliko mtu mwingine yeyote.
Upande huu hufanya mtu akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya.
Kwa uhusiano wowote, huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi. Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu.
Mapenzi ya kibinafi humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na kujidhamini.
Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana.
Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi.
Uchambuzi na ufahamu wa mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali.
Mwanadamu anaweza penda ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe. Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo.
Lazima kama mwanadamu kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani. Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine ilituweze kuishi maisha marefu.
Kama binadamu, mapenzi ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine.
Tukiweza kushikilia aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti yaenziwe na kila mwanadamu.
No comments