Soma Hii Kama Kuna Mtu Amekuvunja Moyo Wako
Anafikiria nini. Nani kampa haki ya kukuvunja moyo? Rudisha moyo wako, hizo ni fikra tu , moyo wako haujavunjika hata kidogo
Mwonyeshe kuwa kuna kitu amekikosa kwako. tengemeza nywele zako, safisha kucha zako , Vaa vizuri, tazama wakati ambapo anakuona jinsi gani uko sahihi, atarudi kukutaka msamaha, Atajisikia kukosea, hataamini kwa kitendo alichokifanya. Atajilaumu kukuacha. Ni kama ulivyojilaumu kumpenda yeye na kufikiri kuwa yeye ndiye pekee hapa Ulimwenguni.
Kumbuka mtu kama huyo hastahili kupata msichana mzuri na smart kama wewe. ni wa muhimu kabisa. Ni moja ya vijana wasio na maana , wenye mchezo na mioyo ya watu. Alikuomba mtoke naye , na ulienda kwake kwa kuwa ulifikiria ni mtu mwema. Lakini akabadilika na kutaka kuchezea akili yako na kukutumia. Ni kama alivyo wa kipekee? ni wa msingi sana. Anafikiria yeye ni nani? mr. basic. kama ukiniuliza mimi.
Huhitaji mwanaume wa muhimu katika maisha yako. Unahitaji mwanaume ambaye ni mkarimu, mpole, mwenye hamasa, mwenye kujali, mwenye usikivu na wewe. huhitaji mtu ambaye ni muhimu na pale pale anaboa. Utakapopata mtu, ambaye ni wa kweli mwenye imani , mwenye kukutaka, mwenye shauku na wewe. hutajisikia kutopendwa maishani mwako.
Unaweza kuwa unafikiria kuwa hakuna mwanaume kama huyo.Wapo. unaweza kufikiria kuwa nadanganya, ni kweli wapo, wanaume wakweli wapo. lakini ni vigumu kuwapata. lakini utampata mmoja , na ukimpata utafahamu kuwa yeye ndiye.
Njia ambayo utafahamu kuwa ni mwanaume mkweli, ni jinsi atakavyokuambia ukweli, kuongea na wewe, kutembea na wewe na kukujali kama mwanamke. Yule ambaye amekuvunja moyo alikuwa ni fake. Alikuwa anataka kitu na mara akipata anakuacha mara moja. Hawa wa kweli wapo na utakutana nao. Atang’ang’ana na wewe kwa mazuri na mabaya.
Najua nakuambia haya, lakini yanapitia sikio la pili na kuondoka, kwa sababu umechanganyikiwa kutokana na huyo aliyekuvunja moyo. Niamini mimi itakuwa rahisi. Utaenda kuelewa kitu fulani cha kupendaza kuhusu yeye. na utakapoelewa utaumia moyo. Halafu utajisikia kama mjinga.
Sikulaumu hata kidogo. Kila mtu hupitia huko kwa kufikiria kuwa ni mtu bora kumbe ni mtu fulani mjinga na tunajiona kama wajinga fulani kwa kumwamini mtu kama huyo. Kila mtu hupitia hisia hizo. Nasema hivyo kwa sababu unapomtazama mwingine unakuwa unakumbuka kitu kilichotokea huko nyuma. Kitu hicho kitakulinda usikutane tena na wanaume wenye mchezo huo.
You are beautiful, Smart and amazing. Utapata mwanaume wa kweli . Yuko mahali fulani. subiri tu wakati ukifika kwa kuwa na yeye anataka kupata msichana mkweli , mzuri kama wewe. Kwa hio amka . jikubali, jipende, jijali. Kuhuzunika ni muhimu katika mahusiano. Huzunika uwezavyo lakini huzuni hio isikuchukue muda mrefu. Lia tu kuhusu huyo mtu aliyekuvunja moyo, Lakini pia kumbuka kuwa sio wanaume wote wako kama huyo. Na utampata mwanaume wa kweli. Mwanaume wa maisha yako.
Umeipenda makala hii?
No comments