Njia sahihi za kutatua migogoro ya kimapenzi
Siku hazisimami, daima zinasonga mbele kwa mbele. Mungu ambaye ndiye mfalme wa kila kilichomo mbinguni na ardhini, anawezesha mabadiliko ya kutisha ndani ya sayari ya dunia. Hakukosea Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ alipoimba Siku Hazigandi.
Kwa kila nukta tunayoivuka, mabadiliko yanayotokea, neema zinazotufikia,
mitihani inayotukabili, hatuna budi kumshukuru yeye muweza wa yote.
Hakika, mimi na wewe binadamu ni viumbe dhaifu, kwa hiyo hatuna ujanja
wa kufanya jambo lolote, isipokuwa kwa matakwa yake.
Tunayatazama mapenzi. Tunatoa mada nzuri ambazo lengo lake ni kukuzindua
wewe msomaji wangu ili ufanye tafakuri ya kina kuhusu uhusiano wako.
Uziangalie hatua zote ulizopita wewe na mpenzi wako kila siku. Naamini
kuwa unajifunza na unafanikiwa.
Aidha, shabaha ya kila mada ni kutengeneza mwanzo wa kikomo cha mateso
kwenye mapenzi. Hii ni kukuweka sawa, kuangalia machungu ambayo kwa
maana moja au nyingine yanakukabili, hivyo ujipange upya, kurekebisha
pale ulipojikwaa kisha unafungua ukurasa mpya ambao hautakuumiza tena.
MIGOGORO, neno hili linamaanisha nini?
Tafsiri: Migogoro ni neno linalomaanisha wingi wa mgogoro ambalo
linatafsiriwa kama hali ya kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi.
Pia inawezekana ikawa ni sura ya fujo.
Tunapoizungumzia migogoro, kwa hali yoyote ile haiepukiki. Na unapoitaja
katika uhusiano ni tatizo lisilo na mwenyewe. Maana ya kusema hivyo ni
kuwa kila mtu aliye ndani ya ndoa, uchumba au vinginevyo analia kwa
staili yake.
Sababu ya kusema hivyo ni kwamba migogoro ni sehemu ya maisha ya kila
mtu ambaye yupo katika uhusiano. Kuna usemi wa Kiswahili kuwa vikombe
ndani ya kabati vinagongana, itakuwa watu wawili waliopitia makuzi
tofauti?
Hivyo basi, usemi huo ndiyo unaothibitisha uwepo wa migogoro katika
uhusiano wa kila mtu, ingawa inatofautiana ukubwa kati ya mtu na mtu,
kulingana na staili ya maisha ya wahusika.
Sambamba na hilo, jinsi ya kutatua migogoro ni kipimo kingine
kinachochangia utofauti kati ya uhusiano wa mtu mmoja hadi mwingine.
Inawezekana pia, hasira, busara na ustahimilivu ulionao ukawa chachu ya
wewe kutofautiana na jirani yako.
Sababu hiyo, pia inayo matawi mengi, mojawapo ikiwa kuvunjika kwa
uhusiano wa kimapenzi, au kufikia kipindi ambacho makosa yanakuwa
hayagawanyiki huku kila mmoja anakuwa hataki kukubali kosa.
Kimsingi, silaha ya kwanza inayoweza kuuokoa uhusiano wowote ule, ni kwa
wapenzi wawili kukubali kuwa na wajibu sawa katika kutafuta suluhu ya
migogoro yao. Nafikiri hapo tuko pamoja!
Kikubwa ni kuelewa kuwa ni watu wawili ambao hufanya uhusiano wao uwe
wenye afya, pia ni katika idadi hiyo hiyo ambayo husababisha penzi lao
lisifike popote. Sababu ni ipi na utofauti huu unasababishwa na nini?
Penzi ni fumbo zito, ndiyo maana huwaunganisha hata wale watu wenye
njozi zinazosigana. Inawezekana kicheche akadumu kwenye penzi lake mpaka
watu wakashangaa, wakati mtu anayesadikiwa ni mtulivu akawa anahama
uhusiano mmoja kwenda mwingine kila siku.
Hata hivyo, muhimu ni kujua mbinu ‘tekniki’ za kutatua migogoro
No comments