TUACHENI TABIA HIZI NI MBAYA KATIKA MAISHA YETU
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!
Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.
Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.
Jikoni ndo shida iliposhika hatamu! Mivyombo ya plastiki imepaukiana imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto. Mahotpot yamekata roho imebaki kuwa sufuria we unalo tuu. Mxiuuu
Ndoo hata hazitumiki zipozipo tu, hata maua hazifai kupandia we unazogo tu huchomi, hutupi wala huzihitaji.. Sa zanini hapo??
Vyombo vya udongo vina mapengo na magego kama vinang'atwaga au vinapiganaga vyenyewe. . Isitoshe kila kimoja na dizaini yake havifanani coz seti imeshavunjikavunjika hivo ndo vimebaki. Unaboa...
Dressing table imejaa mikopo na mibox haina Kazi, perfume ya mwaka 2000 unayo hapo kisa ukumbusho wa zawadi. Ushamba huooo...
Stoo yako mwenyewe ila unaiogopa kuingia coz imejaa vitu visivyohitajika imekuwa ghetto la panya na nyoka kama sio nge badala Ukiweka mnavyohitaji. Ipo siku mtakuta mamba humo..
Nje ya nyumba kuna gari la urithi la babu lipogo tu hapo linafuga ndege na vibaka... Aaalaaaa
Kutupa vitu visivyohitajika hamtupi eti Dhambi na kugawa hamgawi coz mmeviharibu hadi mwisho mtampa nani? Kutwa mnapishana mahospitalini mnaumwa mafua na vifua kila siku.
Kwann msiumwe na mnakaa dampo ? Hivi mnajua km huu ni ugonjwa? Unaitwa hoarder disorder. Tena mnawaambukiza watoto wenu kwani wanajua kwao hata kikopo cha icecream hakitupwagi kinaoshwa kinawekwa hapo.
Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa?
Kama umemind natuma tena
No comments