Kwanini Mwanaume Hufa Mapema Kuliko Mwanamke??
Nimetafakari mwenyewe naona kama majibu hayakuji, au kuna maandiko pengine yanasema mwanaume atakufa mapema kuliko mwanamke?
Kuna wengine nimepata kusikia wanasema eti mwanaume akipiga bao moja anapoteza dakika 3 za kuishi na wanasema hiyo ni kisayansi naamini humu wanasayansi wapo wengi watanitoa tongo tongo.
Ukitazama katika jamii wanawake waliofiwa na waume zao ni wengi kuliko wanaume waliofiwa na wake zao, hiyo imekuwa kama kawaida hivi hata wanawake katika kusisitiza waume zao kuwekeza katika assets huwa wanatumia msemo wa "Baba chanja kuna Leo na kesho usijetuacha tukawa tunateseka". Sasa hebu tuambiane ni kisayansi, kimaandiko au ni mazingira yanapelekea mwanaume anakufa mapema kuliko Mwanamke????
Karibuni kwa hoja
No comments