Mke Amemuacha Mumewe Kisa ni Handsome



Leo July 11,2018 nakupitisha kwenye stori hii inayotoka nchini Saudi Arabia ambapo unaambiwa kuwa Mwanamke mmoja Raia wa Saudi Arabia amemuacha Mume wake sababu ikiwa ni ni mzuri sana (handsome).

Mwanamke huyo ambaye jina lake halijaanikwa hadharani amedumu kwenye ndoa na Mumewe huyo kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo amesema kuwa alikuwa akiishi kwa wasiwasi kutokana na kuhofia kunyang’anywa na Wanawake wengine.

Inadaiwa kuwa kutokana na uzuri wa Mumewe, Mwanamke huyo amekuwa na wivu sana na kushindwa kumuamini kabisa Mumewe akihisi kuwa huenda atakuwa anachepuka na Wanawake wengine ambao watakuwa wanachanganyikiwa na uzuri wake.

Aidha Mwanamke huyo amesema kuwa ameamua kufikia maamuzi hayo ili aishi kwa amani maana kuishi na Mume wake huyo ambaye ni daktari kulikuwa kunampa msongo wa mawazo na kumfanya awe na wasiwasi kila wakati.

No comments