Taraji Afunga Ndoa ya Siri na Mpenzi Wake wa Muda Mrefu



Taraji Afunga Ndoa ya Siri na Mpenzi Wake wa Muda Mrefu MUIGIZAJI maarufu nchini Marekani, Taraji P Henson amefunga ndoa ya siri na mpenzi wake ambaye inasadikika walikuwa na uhusiano wa takriban miaka miwili, Kelvin Hayden.

Tetesi za ndoa hiyo ya kisiri zilizienea baada ya Taraji na familia yake kwenda kufanya hafla ya harusi yao wiki iliyopita, nje ya mji uitwao Anguilla kisha kuposti picha akiwa na mume wake na kuandika maneno haya;

“Mimi na mume wangu.” Akiashiria kuwa, Kelvin Hayden hakuwa mchumba tena bali ni mume wake. Hata hivyo, hadi sasa hakuna picha yoyote inayowaonesha wakiwa katika mavazi ya harusi zaidi ya ile aliyoposti mwenyewe Taraji kwenye Instagram yake.

Taraji anaongeza idadi kwa kuwa msanii wa pili nchini humo kufunga ndoa ya kisiri, wa kwanza akiwa ni ya Cardi B na Offset ambao walifunga ndoa yao mwaka jana.

No comments