Faida na Hasara za Wapenzi kutambulisha Uhusiano Wao.
Watu
wengi hupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi ulio wazi mbele ya jamii.
Kitaalamu hili ni jambo jema, lakini linahitaji umakini katika
kulitekeleza
Wapenzi
wengi nyakati hizi wamekuwa wepesi mno kuiweka wazi jamii juu ya
uhusiano wao bila kujali faida na hasara zake. Ni rahisi kukutana na
watu wa jinsia mbili na kupata utambulisho huu: “Huyu ni mpenzi wangu,
mchumba wagu naomba, umsalimie.”
Tafiti
za masuala ya mapenzi zinaonesha kuwa miongoni mwa mambo
yanayowafurahisha wanawake wengi nyakati hizi ni utambulisho. Dk. Robin
Baker mshauri na mwanasaikolojia nchini Uingereza anathibitisha hili
kwenye uchunguzi wake.
“Kwa
nini hujanipeleka kwenu? Mbona hutoki na mimi kwenye mapumziko yako na
rafiki zako mwishoni mwa wiki? Jamani napenda twende wote klabu.” Hizi
ni kauli za kiu ya utambulisho wa uhusiano kwenye jamii.
Nikiweka
sawa mwenendo wa mada hii, nisiwatenge wanaume kwa mbali, kwani nao
hutajwa kuwa ni hodari wa kutangaza uhusiano wao na wasichana hasa
warembo au wenye nafasi fulani kwenye jamii, lengo likiwa ni kujisifu na
kuuambia umma kuwa “mmiliki wa mali ni mimi.”
Kama
nilivyotangulia kusema, hilo ni jambo jema, lakini swali linabaki
kwenye swali nani ajuaye faida na hasara za uhusiano ulio wazi kwenye
maisha ya mapenzi? Bila shaka akili yako msomaji inatafuta majibu!
Rejeo
la Utafiti wa Taifa la Waingereza linaonyesha kuwa wanawake wanane kati
ya kumi na wanaume sita kati ya kumi walikiri kuwa udanganyifu kwenye
uhusiano wao wa kimapenzi.
Hoja
inayozaliwa kwenye utafiti huo ni hii: “Kuna faida gani kumtambulisha
mpenzi mdanganyifu kwenye jamii?” Labda kabla ya kwenda huko tupitie
faida za uhusiano wa wazi ambazo ni:Kujenga uaminifu, kuthibitisha
chaguo, kufungua ukurasa wa kujisahihisha, kujifunga kwenye ramani ya
penzi la kweli.
Baada
ya kutazama faida tusonge hatua moja mbele kutazama hasara ambazo
nyingi zimeanishwa na Dk. Robin kuwa ni za kisaikolojia. Inaelezwa
kutambulisha penzi la mdanganyifu ni sawa na kupanda mti wa uchungu pale
penzi litakapovunjika.
Ifahamike
kuwa kadiri idadi ya wanaofahamu uhusiano inapokuwa kubwa ndivyo
maumivu ya kuachana yatakavyokuwa. Jaribu kufikiria mtu ambaye
umemtambulisha kwa wazazi, ndugu na marafiki halafu anakusaliti
utawaambiaje uliowajulisha?
Ni
wazi litakuwa jambo gumu kuwaambia wote, hii ina maana utakuwa utajiona
mnyonge kila siku, wakati mwingine si kwa ajili ya kusalitiwa kwako
bali kwa sababu rafiki yako amekutumia meseji ya kukuuliza hali ya
mwenzako.
Nashauri
wapenzi wasitambulishane haraka haraka bila kuchunguzana vinginevyo
wakisalitiwa watapata ugonjwa wa moyo. Ni nafuu kuachana na mwanaume
asiyejulikana kwa marafiki zako, kuliko uliyemtambulisha kwa mbwembwe
kwa ndugu zako na kuonekana naye mtaani kila siku.

No comments