kufanya map3nzi ukiwa na ujauzito, DR LOVE ameeleza kwa kina hapa



Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri.

JE MWANAMKE MWENYE MIMBA ANAWEZA KUENDELEA KUFANYA TENDO LA NDOA?

Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni (fetus)
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda wote wa ujauzito.

JE NI WAKATI GANI MAMA MJAMZITO HARUHUSIWI KUFANYA TENDO LA NDOA?

Ni pale tu mwanamke anapojisikia kuwa na bleeding au maumivu yoyote au leakage ya majimaji yajulikanayo kitaalamu amniotic fluid

Na kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.
Pia kama una historia ya tatizo la cervix

Kumbuka!
Pia ifahamike kwamba si wanawake wote wakiwa na mimba hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke mwenye mimba hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza, then hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri mtoto kuzaliwa.

Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke mwenye mimba husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu huwa nyingi sana kuzunguka uke na hivyo kuwa sensitive zaidi kuliko akiwa hana mimba

Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye mimba anahitaji mikao au milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.

KWA HAYA NA MENGINE HAKIKISHA UMENICHEKI INSTAGRA NAITWA @DAKTARI_WAMAPENZITZ

No comments