Kwa Mtu Asiyekupenda
Hutakuwa mkamilifu kwa moyo ambao sio sahihi.
Hutaweza kupata utulivu kamwe ukiwa na moyo ambao haudundi kwa ajili yako. Macho yako hayataona upendo ndani ya roho inayotafuta mtu mwingine.Unaweza kuwa unasikia kila kitu unachotaka kusikia, Lakini hutahisi hicho kwenye mifupa yako.
Wewe utakuwa ndio mtu ambaye unakumbatia kwa muda mrefu . Atakubusu wakati ambao utakuwa umesahau. Unaweza kuwa umeandika barua za mapenzi nyingi, Lakini hataweza kuelewa kilichopo ndani ya maneno yako. Unaweza kuonyesha hisia zako kwa njia tofauti, lakini hataweza kukuamini.
Halafu utaanza kuwa na sababu. Mwanzoni hutaelewa kama unafanya hivyo. Sababu itakufanya ujisikie vizuri kwa muda mfupi. Utaanza kujiambia kuwa yuko busy, au ndivyo alivyo. Ana vipaumbele vingi. kwa hio ungeweza kushukuru kuwa ni moja kati ya hizo. Lakini pamoja na hayo ni mtu wa siri sana. Kwa hio ni bora kuelewa kuwa hizo sababu zako hazina maana yoyote kwake.
Halafu utaanza kujilaumu mwenyewe. Unaanza kufanya kazi kwa bidii ili ujihakikishe wewe na mwenzako. Utakuwa ni mtu wa kwanza kuomba msamaha. Hata kama hukufanya kosa lolote. Utaanza kumridhisha ili kupatikane amani.Utaacha kusema vitu ambavyo vinakukera.Hutahitaji tena kutata ukutane na mahitaji yako. badala yake utataka huyo mtu akutane na mahitaji yake.
Halafu utaanza kushangaa hata katika kufanya yote hayo bado tu haridhiki. Hakuna hata siku ameamka na kuonyesha upendo unaohitaji. Kusema kweli hakuna siku ambayo atafanya kitu kwa ajili yako. Anaweza kukuacha bila ya kukuaga au kusema hata neno moja. Ukimya wake una nia. Inakukumbusha kuwa humfai na hutaweza kuwa. Hakuna hata maelezo ya kutosheleza.
Usimlaumu kwa kutokukupenda . Huenda alifikiri anakupenda lakini baadae alitambua kuwa hakupendi. Au alijiona hajajitosheleza kwako.
Upendo sio kitu cha kuchambua, Utafahamu tu kama mtu anakupenda.
Hawezi kuondoka mambo yanapokuwa magumu au wakati kunapotokea maumivu ya aina yoyote. hujifunza kutokana na hayo. hufanyia kazi mahusiano. Anafahamu kuachana haikubaliki. kwa hio hupigania ili kuweka mambo sawa.
Hizi ndio nyakati ambazo unaweza kuzitambua. Usijilaumu kwa kuvunjwa moyo kwenye hisia zako, umefanya nafasi yako . Wewe ni mtu mzuri, unaweza kupigania kitu , lakini kama kimeshindikana usijilaumu.
Jikumbushe kuwa Ingawa kuwa peke yako Inaudhi , Lakini kuwepo na mtu ambaye hakupendi kwa ukweli, Ni mbaya zaidi.
Endelea kukazana kujipenda mwenyewe. Ipo siku utapata mtu atakayekubali upendo ulionao. Kuanza kujilaumu utapoteza muda wako na itakurudisha nyuma. Umejitahidi kwa ubora wako, achilia uwe huru.
Hakuna mahusiano ya kufanana. Hakuna ukweli kwamba kuna soulmate mmoja. Mahusiano mazuri ni kila mtu kuwajibika upande wake, kuwa na huruma kwa mwenzake , kusameheana. Yanatengenezwa na watu wawili ambao kila wakati hukutana pamoja kwa upendo. Hata wakati ambao sio mzuri kwao. Wanayapiga mawimbi kwa pamoja. Hii haina maana kwamba kuna mtu sahihi sana Ulimwenguni anakusubiri ili mkafurahie maisha pamoja. Ina maana kwamba kuna mtu kule ambaye anatafuta mahusiano yaliyokamilika na kufahamu kwamba hayawezi kuja kwa urahisi. Wamepitia maumivu pia katika kuelewa kwamba mahusiano yanahitaji umoja ili yawe na nguvu unapoaamua kuanzisha.
Siku moja utakutana na mtu ambaye atachagua kukaa kwako. Mwenye kujielewa. mwenye kujua kuwa mahusiano sio kitu cha rahisi. Ni kitu cha kufanyia kazi.
No comments