Ndoa Nyingi Zinavunjika Kutokana Na Mambo Yanayoweza Kuzuilika
Unapouliza Sababu kubwa ambayo inasababisha ndoa kuvunjika , watu wengi utasikia wakisema, Ni kwa sababu ya Utofauti wao, wamekua mahali tofauti.Hakuna kitu ambacho ni cha kawaida. Ingawa wengi hawaelewi kwamba kuna sababu za kuzuilika.
Kutokana na uchunguzi uliofanyika ,ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya kuwa na uchumi mbaya. Karibu asilimia 20 wanasema hivyo kuwa Pesa ndio chanzo.Lakini kwa nini? Ikiwa watu wengi watafahamu kipato cha mwenza kabla ya kujiingiza kwenye Kiapo. Kuweka sawa matarajio yao, kukubaliana katika mahitaji yao. Inakuwaje tena hawa watu washindwe kuelewana kwa sababu ya pesa? Inakuwaje washindwe kutimiziana?
Fikiria hivi vitu ambavyo vinawaweka hawa watu pamoja: Wanashirikiana interest zao, vipaumbele vyao, mtindo wa maisha walionao. Kitu watu wanachosahau ni au kutambua ni kwamba jinsi unavyoitumia pesa yako ndivyo ilivyo sehemu kubwa ya maisha yako. Lakini, Pia ni jinsi gani unavyotumia weekend yako, Tabia ya uchumi sio kitu ambacho utagundua kwa urahisi unapokuwepo kwenye mahusiano ya mwanzo.
Hio ni kweli kwa sababu kama mwenza wako yuko vizuri katika kuficha idadi ya pesa alizonazo utajuaje kiasi alichonacho?
Kufahamu hilo jambo la pesa , inaondoa tofauti zote, bila ya kufikiria kitu kingine, kuliko wale ambao wanaficha hata kabla hamjaoana, hujui mwenza wako ana kipato gani, huo ni ujinga mkubwa . Ndio maana pesa inasababisha kuvunjika kwa ndoa.
Wanandoa Wenye Mafanikio ,Walijua Haya Yafuatayo kabla ya Kuoana.
Wanafahamu kiwango cha kipato cha mwenza
Wanafahamu malengo ya wenza wao
Wanafahamu matarajio na hamu ya wenza wao
Wanakuwa tayari wamejaa taarifa kamili kuhusu ndoa
Wanakuwa wamekamilika kila mahali, wanajipenda, wanajijali, wamejikubali
Hio ndio njia ya kuwapenda na kuwajali wengine.
Ni waelewa. kila mtu anamuelewa mwenzake.
Unaweza kushangaa kama nikikuambia kuwa mawasiliano ndio Msingi mkubwa katika kujenga mahusiano mazuri na yenye ufahamu mzuri. Pia ni vizuri kumuuliza mwenza wako maswali ya kutosha . Ili tu kuwa na uhakika kufahamu majibu yote. Ni zaidi ya mapenzi kama utajua historia ya pesa yake.
Kwa hio , kabla ya yote hakikisha unakaa na mwenza wako kuongelea masuala haya ya kipato, sio kufurahia chupa ya wine kila siku na kuondoka bila ya kujua kitu. Tambua kuwa unataka kuelekea katika safari ya pamoja, miaka 10, 20, 50, ni muda mrefu. Mazungumzo haya ni kama changamoto zingine za kuwekea msingi wa Imani yako kati yenu. huyo ndiye mtu unayempenda, hakikisha mnaongea hayo mambo yote.
Hakikisha mko katika ufalme mmoja, katika masuala ya kiroho, sio mwingine ufalme wa giza na mwingine ufalme wa Nuru. Mzungumze kuhusu maisha , mkubaliane , na kama itaonekana kuwa hakuna makubaliano, hakuna kulazimishana. Na mahali pa makubaliano ni katika akili zenu.
Baada ya makubaliano yote. Sasa mwili wa mke unakuwa sio mwili wake bali ni wa mwanaume, vivyo hivyo mwili wa mwanaume unakuwa wa mwanamke.
Ukweli na uadilifu , ushirikiano, kuelewana, kuwajibika, kupendana kwa dhati, bila sababu.Kuchaguana kila siku.
Suala ambalo ni la kuzuilika ni kuacha yafuatayo.
Marafiki wabaya
Uvivu
Uchungu na Hasira
Kukosa Uvumilivu.
Makubaliano yakikaa vizuri, mazungumzo mazuri, kipato kikieleweka hakuna ndoa itakayovunjika.
Nakutakia mafanikio katika mahusiano yako.
No comments