Mambo 15 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda - Mtizamo Kutoka Kwa Wanawake
Hebu tuseme ukweli, kuna wakati
mwingine ambao wanaume wanashindwa kuwaelewa wanawake. Unaweza
ukamwaproach mwanamke huku ukijua wazi hutatoboa lakini unashangazwa
mwanamke kama huyo anakukubali fasta.
Na wakati mwingine utaapproach
mwanamke ambaye unaamini kuwa ni rahisi kabisa kumtongoza lakini
ukirusha nyavu badala ya kushika samaki inanasa mawe (sitaki kusema
kinachotokea wakati mwanamke anakuzima mbele ya hadhira)
...halafu sasa kuna wale marafiki zetu ambao kila wakati wao wakitongoza wanakataliwa. (inauma sana)
Well, usitie shaka tena coz hivi
karibuni kama Nesi Mapenzi tumekuwa tukitafiti kwa kuuliza wanawake ni
mambo gani ambayo yanawavutia sana kutoka kwa wanaume na mambo ambayo
yanaweza kuwafanya wafall in love na wanaume na haya ndio mambo ambayo
waliyazungumzia sana:
#1 Kuvalia nadhifu
Kulingana na wanawake ni kuwa
mwanaume anapaswa kuvalia nadhifu kila wakati. Hii ni muhimu kwa
mwanaume kwa kuwa huwezi kujua ni wapi au lini unaweza kukutana na
mwanamke wa ndoto yako. Ni jambo muhimu la kuzingatia lakini masikitiko
ni kuwa ni wanaume wachache ambao huwa wanaona umuhimu ikija katika hili
swala. Ok. ni hivi, kuanzia sasa hadi milele hakikisha kuwa unavalia
kisafi na kinadhifu wakati wote, jipulize marashi na utumie bidhaa zote
za wanaume ambazo zitakupamba.
#2 Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake
wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo
thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa
siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La.
Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe.
Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize
ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume
ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na
tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.
#3 Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia
wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda
mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na
mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili
ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua
kuzungumza maneno ya kunata. Upo?
#4 Mwili mzuri/shepu
Kama vile ambavyo ungependa
mwanamke mwenye shepu na figa, pia wanawake wanapenda wanaume wenye
shepu. So utafanyaje kama wewe una shepu la duara? Ingia gym, fanya
mazoezi ya kukimbia angalau dakika 30 kila siku. Hii itakufanya uwe na
toni nzuri kwa mwili wako. Si mimi ndio nimesema hivi, ni maneno kutoka
vinywa vya wanawake. Anza mazoezi pindi utakapomaliza kusoma hii post.
#5 Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo
mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye.
Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka
kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni
mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na
wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni
hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha.
Usijilazimishe kama wewe si mcheshi. Mwanamke anaweza kucheka kwa mizaha
ambayo hata haichekeshi kama umemsoma mambo anayoyapenda.
#6 Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo
huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti.
Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia
mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi
kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na
misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa
una haki ya kupaza sauti yako usikike balada ya kukasirika ama kusinyaa.
#7 Kazi nzuri na hela ndefu
Ok. Haya si maoni yangu. Ni mambo
ambayo yametamkwa kutoka kwa vinywa vya wanawake. Lakini ngoja tuseme
ukweli...pesa ni muhimu ikija katika maswala ya mapenzi. Ni hivi! Wewe
hupenda wanawake warembo zaidi kuliko wanawake wabovu. Kweli? Hivyo
hivyo wanawake hupenda wanaume ambao ni matajiri zaidi kuwaliko wale
maskini. Kuwa tajiri na kuendesha gari la kifahari ni advantage kwako
(usitie wasiwasi, haya ni maoni ya wanawake tu. hapa Nesi Mapenzi
tushalizungumzia tatizo hili mara kwa mara, pesa si muhimu katika
kutongoza, ushapu wako ndio muhimu)
#8 Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao
wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa
na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako
basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima
ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila
mtu. Tumeelewana?
#9 Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa
kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye
atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa
anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi
yalivyo ulimwenguni.
#10 Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka
kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je
unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na
ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu na
yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa
kumchumbia au la.
#11 Mwanaume anayejua kuzungumza
Kama tu vile kujua jinsi ya
kutumia ucheshi katika mazungumzo yako, kujua jinsi ya kuzungumza na
mwanamke kwa kutumia Sanaa ya Mazungumzo kama vile banta, miondoko ya
mwili na kuchanganya Programu ya Isimu Ubongo ni muhimu zaidi kwa kuwa
kutamfanya mwanamke kujiskia huru zaidi akiwa na wewe na ni mambo ambayo
mwanamke anatamani kutoka kwa mwanaume yeyote. Sanaa zote hizi ziko kwa
kitabu cha
#12 Tabia ya kuheshimu
Kuwa na tabia ya kuheshimu
wengine vile inavyotakikana. Wanawake wote wazuri hawawapendi wanaume
ambao wanapenda kuwachukulia vibaya wengine. Usiwe mbaya kwa watu
walioko chini yako bila ya kuwa na sababu yeyote. Ukiheshimu wengine nao
pia watakuheshimu. Wanawake huwaona wanaume wenye tabia ya kuwaheshimu
wengine kuwa wanaweza kuwa wazazi wazuri. So hakikisha kuwa unatabia
nzuri wakati wote.
#13 Kuwa mwanaume alpha
Wanawake wazuri huwa kwa mikono
mwa wanaume bora. Hakuna mwanamke atataka kuwa na mwanaume mwoga,
asiyejiamini, asiyeheshimu wengine. Itakuwa ushawahi kugundua kitu
flani, kwa kawaida huwa kuna mwanaume mmoja katika kikundi flani ambapo
yeye anadeti wanawake warembo zaidi ilhali wenzake wanadeti wanawake wa
kawaida. Wanaume kama hawa ndio huitwa alpha.
#14 Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao
wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka
kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha,
ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia
comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi
wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.
#15 Mwanaume mwenye usambamba/ compatibility
Ok. Tatizo kuu linajitokeza hapa.
Mara nyingi mwanaume anaweza kumpendeza mwanamke kwa kila kitu lakini
mwanamke anaweza asikubali mwitikio wako kwa kuwa hamna uwiano ulio
sawa. Mwanamke anaweza kukukataa kwa sababu zake binafsi. Kama unataka
kufanikiwa na hili basi hakikisha kuwa unakuwa mkweli, makinika na
interests zake na usome mambo anayopenda na kuchukia. Kama ataona kuwa
kuna uwiano ndani yenu, basi ni rahisi kwa yeye kukukubali.
Mwisho ni kuwa haya ni maoni
ambayo yametoka kwa vinywa vya wanawake, hivyo kama kuna moja kati ya
haya maoni 15 tuliyoyaorodhesha unayakosa, basi ni muhimu uanze kazi
sasa hivi.

No comments