Soma Hii Kama Kuna Mtu Amekuvunja Moyo Wako
Anafikiria nini. Nani kampa haki ya kukuvunja moyo? Rudisha moyo wako, hizo ni fikra tu , moyo wako haujavunjika hata kidogo
Mwonyeshe kuwa kuna kitu amekikosa kwako. tengemeza nywele zako, safisha
kucha zako , Vaa vizuri, tazama wakati ambapo anakuona jinsi gani uko
sahihi, atarudi kukutaka msamaha, Atajisikia kukosea, hataamini kwa
kitendo alichokifanya. Atajilaumu kukuacha. Ni kama ulivyojilaumu
kumpenda yeye na kufikiri kuwa yeye ndiye pekee hapa Ulimwenguni.
Kumbuka mtu kama huyo hastahili kupata msichana mzuri na smart kama
wewe. ni wa muhimu kabisa. Ni moja ya vijana wasio na maana , wenye
mchezo na mioyo ya watu. Alikuomba mtoke naye , na ulienda kwake kwa
kuwa ulifikiria ni mtu mwema. Lakini akabadilika na kutaka kuchezea
akili yako na kukutumia. Ni kama alivyo wa kipekee? ni wa msingi sana.
Anafikiria yeye ni nani? mr. basic. kama ukiniuliza mimi.
Huhitaji mwanaume wa muhimu katika maisha yako. Unahitaji mwanaume
ambaye ni mkarimu, mpole, mwenye hamasa, mwenye kujali, mwenye usikivu
na wewe. huhitaji mtu ambaye ni muhimu na pale pale anaboa. Utakapopata
mtu, ambaye ni wa kweli mwenye imani , mwenye kukutaka, mwenye shauku na
wewe. hutajisikia kutopendwa maishani mwako.
Unaweza kuwa unafikiria kuwa
hakuna mwanaume kama huyo.Wapo. unaweza kufikiria kuwa nadanganya, ni
kweli wapo, wanaume wakweli wapo. lakini ni vigumu kuwapata. lakini
utampata mmoja , na ukimpata utafahamu kuwa yeye ndiye.
Njia ambayo utafahamu kuwa ni mwanaume mkweli, ni jinsi atakavyokuambia
ukweli, kuongea na wewe, kutembea na wewe na kukujali kama mwanamke.
Yule ambaye amekuvunja moyo alikuwa ni fake. Alikuwa anataka kitu na
mara akipata anakuacha mara moja. Hawa wa kweli wapo na utakutana nao.
Atang’ang’ana na wewe kwa mazuri na mabaya.
Najua nakuambia haya, lakini yanapitia sikio la pili na kuondoka, kwa
sababu umechanganyikiwa kutokana na huyo aliyekuvunja moyo. Niamini
mimi itakuwa rahisi. Utaenda kuelewa kitu fulani cha kupendaza kuhusu
yeye. na utakapoelewa utaumia moyo. Halafu utajisikia kama mjinga.
Sikulaumu hata kidogo. Kila mtu hupitia huko kwa kufikiria kuwa ni mtu
bora kumbe ni mtu fulani mjinga na tunajiona kama wajinga fulani kwa
kumwamini mtu kama huyo. Kila mtu hupitia hisia hizo. Nasema hivyo kwa
sababu unapomtazama mwingine unakuwa unakumbuka kitu kilichotokea huko
nyuma. Kitu hicho kitakulinda usikutane tena na wanaume wenye mchezo
huo.
You are beautiful, Smart and amazing. Utapata mwanaume wa kweli . Yuko
mahali fulani. subiri tu wakati ukifika kwa kuwa na yeye anataka kupata
msichana mkweli , mzuri kama wewe. Kwa hio amka . jikubali, jipende,
jijali. Kuhuzunika ni muhimu katika mahusiano. Huzunika uwezavyo lakini
huzuni hio isikuchukue muda mrefu. Lia tu kuhusu huyo mtu aliyekuvunja
moyo, Lakini pia kumbuka kuwa sio wanaume wote wako kama huyo. Na
utampata mwanaume wa kweli. Mwanaume wa maisha yako.
Umeipenda makala hii?
No comments