Mazoezi 12 Ya Kuongeza Nguvu Za Kiume
Nguvu za kiume
huhusisha mambo mengi. Hayani pamoja na, hamu ya mapenzi; kusimama kwa
uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la
ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa
mwili katika kutenda tendo lenyewe. Kuna viungo vingi mwilini
vinavyohusika na nguvu za kiume.
Viungo hivi ni kama
ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya
uume iitwayo corpora cavernosa na kadhalika. Kukosa nguvu za kiume ina
maana kuwa kiungo kimoja kati ya viungo vyote husika hakifanyi kazi kwa
mfano figo yaweza kukosa kufanya kazi hivi basi kusababisha kukosa nguvu
za kiume.
Kuna mambo kadhaa
yanayosababisha ukosefu wa nguvu za kiume kwa mfano kupatwa na maradhi,
vyakula unavyokula na mtindo wa maisha huweza kufanya viungo kutofanya
kazi. Baadhi ya maradhi hayo ni ugonjwa wa sukari, presha ya kupanda,
presha ya kushuka.
Tabia zinazosababisha
viungo kutofanya kazi ni kama uvutaji wa sigara, kuchelewa kulala,
kutopata usingizi, kujinyanyua, unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa ya
kulevya au kufanya kazi kupita kiasi hivi basi kukosa wakati wa
kupumzika. Sababu nyingine ni kama kutumia nguvu nyingi kusukuma choo
kwa sababu ya tatizo la kusukuma choo, kutokunywa maji, uzito mwingi,
kitambi na hasa kutofanya mazoezi.
Kuna njia nyingi za
kuongeza au kurejesha nguvu zako za kiume kwa mfano unaweza kubadilisha
vyakula unavyokula kama kula nafaka zilivyo na nyuzi nyuzi kwani nafaka
husaidia kuongeza homoni za kiume, kula asli, kula matunda mengi, kula
tangawizi, kunywa vanilla na kunywa maji mengi.
Njia nyingine ni
kumtembelea datary na kumwambia shida yako, anaweza kukupa tembe au
akudunge sindano kama njia ya kukusaidia njia ya mwisho na ambayo
tunazungumzia ni kufanya mazoezi ambayo husaidia uongeza nguvu za kiume.
Kati ya njia hizo zote hakuna ambayo utapata matokeo yake kwa siku
moja, utahitaji kufuatilia njia hiyo na kuwa na uvumilivu na imani kuwa
utasaidika mwishowe.
Kuna mazoezi mengi ambayo husaidia kurejesha nguvu za kiume kwa mfano:
1- Kujiinua pande ya juu ya mwili
Zoezi hili huhitaji
uweke mpira wa zoezi chini na uwekelee mguu wako juu yake huku ukitumia
mikono yako hushikilia upande wa juu wa mwili wako.
Hujaribu kuonyesha kuwa
unapoweza kushikilia mwili wako kwa muda mrefu basi utaweza kuongeza
nguvu zako za kiume zaidi. Sehemu ya mwili inayoongezwa misuli ni
mabega, kifua na upande wa mbele wa mkono pande juu.
2- Kujiinua pande ya chini ya mwili
Aina hii ya zoezi
inahitaji ulale wima kwa mgongo kasha uinue miguu yako hadi kwenye kifua
na kisha ushikee miguu yako kutoka nyma kwa sekunde thelathini.
Rudia jambo hili kwa mara nyingi kama utakavyoweza. Husaidia sehemu ya chini ya mgongo na kutengeneza misuli ya tumbo.
3- Pande ya chini ya mwili
Zoezi hili unafaa
kupiga magoti na kuweka sehemu ya juu ya mwili wima kasha unafaa
kuinamisha sehemu ya juu ya mwili pole pole huku ukiinama zaidi hadi
mahali ambapo utashindwa kurudi nyuma zaidi.
Kaa hivyo kwa sekunde
thelathini kisha upumzike na kurudia zoezi hili kwa mara kadhaa. Zoezi
hili husaidia kuongeza misuli sehemu ya juu ya miguu.
4- Kuongeza nguzu sehemu ya kati ya mwili
Katika zoezi hili
unafaa kusimama huku ukiwa umerudisha mguu moja nyuma na mwingine mbele
na kuinamisha sehemu ya juu ya mwili nyuma.
Miguu inafaa kuwa na
tofauti ya mita moja na kiuno kinafaa kuwa umekisukuma mbele. Baada ya
dakika moja geuza miguu. Zoezi hii husaidia kuongeza misuli ya kiuno.
5- Uvumilivu
Zoezi hili hufanywa kama umelala kwa mgongo huku umekunja miguu yako na mikono ikiwa wima pande zote za mgongo.
Kisha uinue kiuno na
kukaa hivyo kwa dakika kadhaa, zoezi hili husaidia kupima uvumulivu wako
ukiwa umeinua kiuno na kusaidia kuongeza nguvu katika kiuno chako.
6- Kuinua uzito
Kuinua vitu vyenye
uzito ni aina ya zoezi inayosaidia kuongeza nguvu za kiume. Zoezi ya
aina hii husaidia mtu kujiamini kwa chiochote anachofanya hata anapoinua
vitu hivyo vyenye uzito.
Kuinua kwa vitu vizito
kama mawe husaidia kuongeza misuli mikononi hasa upande wa juu, upande
wa mbele. Misuli hio husaidia kuongeza nguvu mwilini.
7- Kutembea
Hii ni aina rahisi ya
zoezi ambayo haihitaji matumiizi ya nguvu nyingi lakini watu wengi
hawapendi zoezi hili. Badala yake watu hupenda kuendesha magari ili
wasichoke.
Kutembea husaidia
kupunguza uziti na kitambi. Vile vile kutembea husaidia kupunguza uchovu
baada ya kufanya kazi ambayo haihitaji nguvu nyingi.
8- Kuchuchumaa
Hii ni aina ya zoezi
ambayo unahitaji kuekelea mikono yako kwenye kiuno chako na kuchuchumaa
hadi chini ambapoutakua umekalia miguu yako na kuinamka bila ya kuondoa
mikono kutoka kwa kiuna na bila kuondoa miguu mahali ilipo.
Zoezi ya aina hii husaidia kuongeza nguvu na misuli pande ya nyuma ya miguu ili kuweza kushikilia mwili.
9- Kuruka
Kuruka ni zoezi nzuri
kwa kuongeza nguvu za kiume. Unaporuka unaongeza miguu yako nguvu na
misuli kwani unapoondoa mwili juu unahitaji kusimama au kujishikilia
vizuri ili usianguke.
Mazoea ya kuruka huhakikisha miguu ina nguvu ambalo ni jambo la muhimu sana katika uongezaji wa nguvu za kiume.
10- Kuogelea
Kuogelea ni tendo la
kuingia katika maji mengi na kutoka mahali pamoja hadi pengine bila ya
kutembea. Kuogelea husaidia mikono na miguu yao.
Unapoogelea misuli ya
miguu na misuli ya mikono yako huongezeka, nguvu vako mwilini huongezeka
kwani unatumia mwili wote katika kuogelea. Miguu husonga na mikono vile
vile hivi basi mishipa ya damu lazima ipeleke damu nyingi mikononi na
miguuni.
11- Kutembea kwa haraka
Hii ni tofauti na
kukimbia na pia ni tofauti sana na kutembea. Kitu cha muhimu kujua ni
kuwa unahitajika kutenganisha miguu yako kwa mbali na kwa haraka.
Unapotenganisha miguu
na kutembea kwa haraka misuli ya upande wa juu wa mguu inaongezeka na
pia mishipa ya damu inasafirisha damu upande wako wa juu wa mguu. Hili
ni jambo la muhimu sana kwani maana moja ya nguvu za kiume ni kuweza
kusimama kwa uume barabara na ili uume usimame unahitaji damu kuwepo.
12- Kulala
Hii si aina ya zoezi
lakini ni muhimu kwa mazoezi niliyoyataja hapo awali. Usingizi husaidia
kupumzisha mwili pamoja na viungo vyote vya mwili. Kupumzisha mwili ni
muhimu ili wakati ambapo unahitaji kufanya chocho uwe na nguvu
zinazofaa.
Usipolala, wakati
ambapo unahitaji nguvu zako za kiume, mwili utakuwa umechoka hivi basi
viungo vyako vya mwili havitatoa matokeo.
No comments