Afya ya Sauti; Unapenda Kuimba? Basi hii ni kwa ajili yako.

760x350-vocalrange
Ieleweke kwamba, Kuwa na utimamu wa kimwili (fitness) sio kuwa bora kuliko mtu flani, bali ni kuwa bora kuliko ulivyokua awali. Watu wengi sana hutumia muda wao mwingi tu katika majumba ya mazoezi (Gym) wakifanya mazoezi mbalimbali ya kimwili na wana nidhamu sana katika hili, ni jambo zuri sana kiukweli. Lakini tunasahau kitu kimoja; Koo lako ni sehemu ya mwili wako pia! na kama ukitenga muda kwa ajili ya mazoezi, na utunzaji mzuri wa Sauti yako, utawashsangaza wengi sana na ubora wa sauti yako! Ungependa kuelewa nini cha kufanya?? TWENDE….
AFYA YA SAUTI:
Sauti yako ndiye balozi wako kwa ulimwengu, umewahi kuona mtu hata awe mpole kiasi gani, lakini kama akiwa na sauti ya kutisha (sanasana wazee) hata watoto humuogopa?? au hata ukifatwa na mtu ambae humjui na ana sauti ya ajabu ajabu we mwenyewe lazima uogope!
Sauti unayoitumia kuongea ndiyo hiyo hiyo unayoitumia kuimba, hivyo basi, ukiitumia sauti yako hovyo katika maongezi utaathiri pia uimbaji wako! Unyevu, Mazoezi ya misuli ya shingo na Mapumziko, ndiyo viungo muhimu katika kuipika afya ya sauti yako. Vinafanyaje kazi? ENDELEA…
UNYEVU;
drinking03-water-tap-ethiopia_13109_600x450
Msingi wa sauti ni maji mengi
Tumia Maji ya Kunywa kwa wingi sana ili kuzifanya Ala zako za Sauti (Vocal Chords) ziwe na unyevu, zisikauke. Maji hulainisha na kuyaondoa makohozi katika koo na kuyafanya yasigandamane kwenye ala za sauti.
Usitumie “spray” ya aina yoyote kunyevusha koo lako. Kumbuka kubadili mazingira yenye hali za hewa tofauti tofauti huathiri ala za sauti. Cha kufanya, kunywa maji ya kutosha na kula matunda yenye maji mengi kama matikiti maji na matango, achana na matunda yenye tindikali nyingi kama “citrus fruits” mfano machungwa, malimao, na ndimu kwani yatazisugua ala za sauti na kuziachia mikwaruzo.
MAZOEZI;
warm-up-exercise
Mazoezi ya sauti yanachekesha, yafanye ukiwa peke yako, hasa bafuni unapooga
Fanya mazoezi ya sauti na mwili kwa ujumla na kwa bidii. Fanya mazoezi ya ulimi kama “tongue trill” (yafanye ukiwa mwenyewe, hasa bafuni ili usije ukachekesha watu) ili kuruhusu upitaji mzuri wa hewa kwenye koo, na upumuaji mzuri kwa ujumla.
Jifanyie pia masaji maalum za ulimi na maungio ya taya, fanya “humming“, yaani tamka herufi ‘m‘ kwa muendelezo, ukiwa umefumba mdomo, (kama sauti ya nyuki wengi) ukiwa bafuni ili kuipasha sauti yako. Hakikisha unafanya hivi kila siku kwa matokeo mazuri.
Fanya pia mazoezi ya misuli ya shingo, koo taya na mabega, pia legeza misuli ya shingo na koo unapoimba noti za juu sana au za chini sana, ukikakamaza shingo itakusababishia maumivu na sauti itaharibika.
MAPUMZIKO;
94317-90736
Baada ya kuunguruma kwa muda mrefu, pumzika
Hakuna kitu kinachoweza kufanya kazi bila kuchoka, hata iwe mashine ya Mjerumani. Kwahiyo, hakikisha unapata mapumziko ya kuongea baada ya kutoka kwenye maongezi au uimbaji uliokufanya utumie nguvu nyingi ili kuinusuru sauti yako.
Epuka tabia za kupiga kelele hovyo, kubishana kwa sauti na nguvu nyingi, au kuimba kwa nguvu nsana kusiko kua na maana yeyote. Epuka sana uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kwani kutakusababishia madhara kwenye sauti.
KWA KUMALIZIA…
  • Acha sauti yako ing’ae, kuwa wewe na usiigize sauti ya mtu
  • Siku zote kunywa maji mengi yasiyochanganywa na kitu, maji tu!
  • Pata muda wa kutosha wa kupumzika, epuka kelele zisizo za msingi
  • Mwisho, Jifunze mbinu bora za uimbaji (tutakuwekea mbinu hizo muda si mrefu)
Picha kwa hisani ya Google.
UMEPATA NINI HAPA? TUANDIKIE COMMENT YAKO, NA USISAHAU KUSHIRIKI NA WENZIO MITANDAONI, IKIWA NI PAMOJA NA WHATSAPP, FACEBOOK, NA LINKEDIN.

No comments