NJIA 10 ZA KUMFANYA MPENZI WAKO ASITOKE NJE YA NDOA AU ASIKUSALITI


1: PUNGUZA KUWA MTU WA KULAUMU KILA MARA
kuna watu huwa wanakosea sana katika mapenzi, wao kila mda ni kumlaum mpenzi wake,
 lawama zinatokanaje?
wengi akiona mpenzi wake hajampigia simu au hajapatikana kitu cha kwanza kwake ni kumlaumu mpenzi wake na kumtolea lugha ya ukali au ata mpenzi wake amemwahidi kitu alafu hajamtimizia yeye ni kulaumu tu pasipo kumuliza mpenzi wake tatizo nini na akaambiwa na akaelewa na kama hujaelewa mwombe akupe maelezo ya ziada na ushahidi kwa upole.
madhara yake nini?
mme au mpenzi wako ukiwa unamlaum kwa kila kitu anaweza akawa siku amekumbana na mambo magumu aidha kazini kwake au njiani, kutokana na hasira aliyo nayo atakuchukia na wewe ukifanya hivyo mara mbili mala tatu utamkosa mpenzi wako atamtafuta mtu atakaye kuwa faraja kwake.

2 USIMUUDHI MPENZI, MME/MKE WAKO
hakikisha kwamba husababishi maudhi ya aina yeyote kwa mpenzi wako,
Maudhi yana sababishwa na nini?
ikiwemo lugha chafu, kumzungumzia na kumsifia mwanaume mwengine, mpambe mpenzi wako kwa majina mazuri (Baby, honey, my sweet, na mengineyo kama hayo) kabla ya tendo. kukasirika kila mda, kutoa maneno ya kumkatisha tamaa mpenzi wako, kebehi, pamoja na lawama kama tulivyo ona hapo juu.
madhara yake nini?
kumfanya mpezi,mke au mme wako kukuchukia kila mda kutokana na maudhi yako. akitokea anaye jua kumpetipeti ndo basi tena kakushinda 

3: TAMBUA THAMANI YAKE
Unapokuwa Umeapa Kuwa Utampenda Mwenzako Hadi Kifo Kitakapowatenganisha, Uwe
Umefanya Hivyo Kwenye Nyumba Ya Ibada Au Kwingine, Lazima Ufahamu Jinsi Ya Kutambua
Juhudi Za Mpenzi Au Mwenzi Wako, Ili Kuepukana Na Uwezekano Wa Mwenzi Wako Kukuona
Kama Vile Unamchukulia Kawaida Na Hujali Jitihada Zake. Mtu Anapodhani Mwenzake
Hajali Jitihada Zake Ni Rahisi Kushawishika Kutoka Na Kwenda Kwa Mtu Atakayeitambua
Thamani Yake.
Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwenzako Kudhani Humjali Wala Kuthamini Juhudi Zake, Mara
Kwa Mara Jiulize Unaweza Kumfanyia Nini Ili Kumwonesha Kuwa Unamtambua. Jambo
Lenyewe La Kumfanyia Linaweza Kuwa Rahisi Tu, Mathalani Kumtumia Ujumbe Mfupi Kwa
Ajili Tu Ya Kumwambia Kuwa Yuko Mawazoni Mwako. Iwapo Utajenga Mazingira Ya
Kuitambua Thamani Ya Mwenzako Mara Kwa Mara Haitakuwa Rahisi Kwa Mwenzako Huyo
Kufikiria Kuchepuka

4:JIFUNZE KUOMBA MSAMAHA UNAPO KOSEA.
kuomba msamaha ni nguzo kubwa ya mapenzi ingawa watu wengi hawajui. unapo tambua mpenzi wako amekasirika jaribu kutumia lugha ya kumshawishi mpenzi wako akusamehe. makosa kwa binadamu ni lazima kutokea lakini je unapo kosea unatumia lugha gani kuomba msamaha? mwambie mpenzi wako "sory beby naomba nisamehe mpenzi wangu sikujua kama nikifanya hivi ntakuudhi mme/mke wangu" hii itamfanya mpenzi wako apunguze hasira na akusikilize. kumbuka unapo omba msamaha na ukasamehewa usije ukarudia kufanya kosa kama hilo.

5:UWAPO CHUMBANI NA MPENZI WAKO
Usafi wa mwili;  Kitu cha kwanza kukizingatia kabla ya yote lazima mwanamke uuweke mwili wako safi kabla ya tendo. Hii ikiwemo na kuoga mwili mzima, kusafisha sehemu zako za siri ikiwemo na mahala popote ambapo pamefichika kwani sehemu hizo wanaume walio wengi na wanaojua mapenzi hupenda kuzichezea sehemu hizo kwakua ndizo ambazo huhifadhi mihemko ya mwanamke. Baadhi ya wanawake hujisahau kujisafisha vizuri na kutoa jasho tu lililopo katika miili yao bila kusafisha sehemu nyenginezo ambazo hutumika katika masuala mazima ya tendo la ndoa huvyo kutokana na harufu za baadhi ya sehemu humpunguzia mwanaume hamu ya kitendo. Hakikisha masikio na kitonvu chako vipo safi. Pia hakikisha sehemu ya magoti yako kwa nyuma zipo safi
mpambe mpenzi wako kwa majina mazuri (Baby, honey, my sweet, na mengineyo kama hayo) kabla ya tendo. Baadhi ya wanawake huwaita waume zao majina mazuri wakati wanapopewa zawadi tu au wakati wanapofikishwa kileleni hii sio sawa kabisa, sababu huu utakuwa ni unafiki mwanaume aweze kukufikisha kileleni anaitaji maandalizi bibi eeh, muandae kwa majina mazuri ili ajisikie furaha mwili upate kutulia kwani wengine huwa wameudhiwa huko walipotoka sasa unatakiwa kumtoa alipo na kusahau kabisa. kwani kitaalamu mwili unapotulia (relax) huondosha msongo wa mawazo hivyo utakuwa umeufanya ubongo wake uweze kukuwaza wewe wakati wote

6: USICHUKIE MPENZI WAKO KUWA NA MARAFIKI NA MARAFIKI
Jambo Jingine Ambalo Linaweza Kumpunguzia Mwanamume Uwezekano Wa Kufanya Mapenzi Nje
Ya Uhusiano Ni Kumhakikishia Urafiki Na Wanaume Wenzake. Kwa Vyovyote Vile, Lazima
Mwanamume Wako Utakuwa Ulimkuta Na Marafiki. Usimzuie Kuendelea Kuwa Nao.
Unapomuunga Mkono Mwanamume Katika Kampani Yake Na Wanaume Wenzake Utakuwa
Umemwongezea Mwanamume Huyu Fursa Ya Kuendeleza Ukaribu Na Watu Wake, Hivyo
Kupunguza Fursa Ya Kujipenyeza Kwa Wanawake Wengine Katika Maisha Yake. Ukimbanabana
Halafu Na Wewe Ukashindwa Kuwa Rafiki Kwake, Akimpata Mwanamke Aliye Tayari
Atashikamana Naye.

 7:JITAHIDI KUWA MWELEWA
Mojawapo Ya Vishawishi Vikuu Vya Mwanamume Kujiingiza Katika Mapenzi Ni Kumpata Mtu
Ambaye Atamwelewa. Kama Huna Sifa Hii, Ni Rahisi Kwa Mwanamume Wako Kutoka Kwa Ajili
Ya Kuitafuta Kwingine.
Ili Kumzuia Mwanamume Kutoka, Onesha Jitihada Za Kutaka Kumwelewa Na Kufahamu
Matakwa Yake Ili Uweze Kuyatimiza. Katika Hili Usiogope Kumuuliza Maswali Magumu,
Mathalani Waweza Kumuuliza “Unajisikiaje Kuhusiana Na Uhusiano Wetu?” Au “Ni Kitu
Gani Ulichokuwa Unakitaka Katika Uhusiano/Ndoa Ambacho Hujakipata Mpaka Sasa?” Namna
Hii Utakuwa Umeonesha Jitihada Za Kutaka Kumfahamu Na Kumridhisha.

8: WAHI MAPEMA KURUDI NYUMBANI BAADA YA KAZI
Baada ya kumaliza kazi mwanaume au mwanamke unatakiwa kuwahi mapema nyumbani na kama utachelewa kutokana na sababu mbalimbali usisite kumtaarifu mpenzi wako. hii itafanya mpenzi wako asiwe na wasiwasi na wewe.

9: MAWASILIANO NI NGUZO KUU YA MAPENZI
kumbuka kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na mpenzi, mkea au mme awapo mbali hii itawasaidia kuimarisha ukaribu wenu. katika mawasiliano hapa naomba niongee kitu. usije ukawa unamudhi mpenzi wako kila akupigiapo simu au umpigiapo, punguza maudhi yasiyo ya msingi hii itamfanya mpenzi wako asijisikie raha ya kuwasiliana na wewe tena na pengine kuzima simu kabisa ili kupunguza maudhi.

 10: USIACHE KUMPATIA MPENZI WAKO ZAWADI.
jambo la kumi na la mwisho ni uhakikishe kila unapoondoka nyumbani au unapo kaa mbali na mpenzi wako usiache kumletea zawadi hasa zile azipendazo. sio tu unapo kaa mbali ata unapokuwa karibu siku mojamoja mfanyie kitu mpenzi wako hii itamfanya mda wote akuwaze wewe tu.
kitu cha kuzingatia hapa. wanawake wengi wanaona mtu anayepaswa kufanya jambo hili ni mwanaume tu. sio kweli. mwanaume pia anahitaji kuletewa zawadi hii itaimarisha uhusiano. ukiacha kumletea mme wako zawadi ukitegemea yeye akufanyie kila kitu utakuwa unakosea akimkuta mtu anayejua kumlinda na kummiliki mwanaume hata kukumbuka tena.
na usiache kushukuru unapo pewa zawadi hata kama ni ndogo au huipendi shukuru tu then utajua jambo la kufanya juu ya hiyo zawadi.

No comments