UKIFANYA KITU HIKI USIKU, ASUBUHI UTAKUTWA UMEKUFA!!
Hapa AFYAKONA, tunajua unajua lakini tunakumbushana mambo ya msingi ili kuonesha tunavyokujali. Leo ningependa kukuletea kitu ambacho kama ukikifanya usiku, basi jua kabisa asubuhi hautaamka, utakua umekufa!Ni kitu gani hicho? Twende sasa…
KULALA NDANI NA JIKO LA MKAA LIKIWA LIMEWAKA
Umewahi kupata taarifa kuwa familia flani wamekutwa asubuhi wamefariki bila hata tatizo kujulikana? Skia; Mwili wa binadamu unahitaji hewa ya Oxygen kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzalishaji nguvu na ukuaji wa mwili kwa ujumla, na pale hewa hii inapokosekana ndani ya muda mfupi, basi binadamu hufa. Unapovuta hewa na kuingia kwenye mapafu, hewa ya Oxygen huchukuliwa hadi ndani ya damu na kusafirishwa na chembechembe ziitwazo Haemoglobin kwenda sehemu zote za mwili ambapo damu inafika, na kuachwa ifanye kazi huko, wakati huo Hewa ya Carbondioxide ikibebwa na chembechembe zilezile hadi kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje kwa njia ya pua au mdomo.
Tatizo linakuja pale ambapo ndani ya mapafu inaingia “Hewa ya Ukaa” (Carbonmonoxide). Hewa hii ni sumu na hujulikana kama “silent killer“ yaani muuawaji wa kimyakimya, inachofanya hewa hii inapoingia ndani ya mapafu, huzuia zile chembe za Haemoglobin kubeba Oxygen na hivyo, Carbonmonoxide ndiyo husafirishwa mwilini, na kibaya zaidi, Hewa hii hua haikubali kutengana na haemoglobin na kusababisha Oxygen ikose kabisa namna ya kuzungushwa mwilini kwa kuwa ‘vibebeo’
vyote vimejazwa! Kwa namna hiyo, taratibu mwili unaanza kukosa Oxygen, kitu kinachopelekea ubongo kuanza kuathirika, chembe hai za mwili kuanza kufa, na hatimaye ndani ya muda mfupi mtu anakufa, tena kimyakimya pasipo hata yeye mwenyewe kujua kuwa anakufa!
VYANZO VYA CARBON MONOXIDE NI VIPI?
thaistove01
Hewa ya ukaa (carbonmonoxide), husababishwa na uchomaji moto wa fueli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkaa, kuni, mafuta ya taa, petroli, makaratasi, majiko ya mafuta, na uchafu mwingine unapochomwa moto.
Ni kiasi gani cha Carbonmonoxide kinaua? Unapolala chumbani ukiwa umewasha jiko la mkaa na wakati huo umefunga milango na madirisha, utasababisha kusiwe na mzunguko mzuri wa hewa inayoigia na kutoka, na kama hewa ya ndani haitoki nje, mtu atakua akitumia ile Oxygen iliyobaki ndani tu, wakati huo jiko la mkaa likiwa linazidi kutoa carbonmonoxide, mwisho carbondioxide inazidi sana, na mtu anaanza kuivuta kwa wigi kuingia mwilini mwake. Hii huwatokea sana wale wanaopenda kupika vitu kama maharage usiku kwa ajili ya kesho, na wale wanaohitaji joto la jiko ndani wakati wa baridi kali usiku.
DALILI ZA MTU ALIYE ZIDIWA NA CARBON MONOXIDE NI;
co
Mafua na kichwa kuuma
Uchovu na Kizunguzungu
Kushindwa kupumua vizuri
Kuchanganyikiwa akili
misuli kukaza na hata kuzimia
Ukishtuka asiku ukahisi dalili kama hizi, kwako au kwa watoto, usirudi tu kulala, hakikisha unaangalia kama kuna jiko limewashwa litolewe nje, na watu hao watolewe nje mahali penye hewa ya kutosha, hali ikizidi kuwa mbaya basi Daktari atafutwe!
Naamini kosa hili halitafanyika, Usisahau kuandika Email yako ili upate habari mpya kila inapotoka, na pia usiache kuweka maswali na maoni yako hapo chini, vilevile tufatilie kwenye kurasa zetu za Facebook na Instagram. Usiwe mchoyo, SHERE habari hizi hadi kwa Whatsapp ili kila unayempenda aelimike pia!
No comments