Fundisha Akili Yako Maarifa Na Ukue Kwa Furaha
Unawezaje kujizuia kuwa na mawazo mabaya ili kuishi ukiwa na mawazo mazuri?
Kustaafu. Mjomba wangu hakutegemea kuwa na mzigo wa akili ambao uliambatana na kukosa kazi.
Siku kwa siku alisema, Nina muda mwingi wa kuwa huru. Akili yangu haiko kwenye hali nzuri. Siwezi kuacha kufikiria sana na makosa yangu yaliopita yameanza kunirudia.
Kama hukuwahi kuajiriwa na hukuwahi kuwa na mambo mengi ya kufanya, Au umewahi kuwa mgonjwa , huenda ukawa unaelewa hali niliyo nayo.
Umetambua hali ambayo mjomba wangu alikuwa nayo , akili ilikuwa inafanya kazi zaidi katika kuchukua hisia zote mbaya. Kila mawazo yaliokuja hayakuwa mazuri. hakuweza kuyathibiti, yalibaki ndani yake. yalikuwa yanazidi kuwa mabaya na kumletea hisia za zenye matatizo.
Kuwa na umri mkubwa ina maana, lakini watu wengi hawana muda wa kukuza akili. Akili inakuwa rahisi kukumbuka mambo yaliopita zaidi kuliko yaliopo, kujilaumu kwingi na woga unazidi kuwa na nguvu.
Unazo mbinu ambazo zitakuwezesha kutunza akili yako iwe na hali nzuri?
Kama umestaafu na hukuwa mtu wa kutafuta maarifa , huwezi kwenda kuishi vizuri, ni kwenda kuteseka kwa sababu hutakuwa na kitu endelevu katika maisha yako. Na kwa sababu hio hutaweza kuwa na furaha.
Wewe sio mtu pekee ambaye umekuwa huna furaha , maisha yako yana mchanganyiko wa furaha na mafanikio yasiodumu, una hisia mbaya, mahusiano yako sio mazuri, au kushindwa na kupoteza nafasi, kuwa na wivu ni kawaida katika maisha ya watu wengi.
Unaweza Kuachana Na Kumbukumbu mbaya?
Unaingiza hisia mbaya kuhusu maisha ya baadae na unachanganyikiwa?
Umri mkubwa unaweza kuleta stress kubwa, Hasa umri wa miaka 60. Kuna changamoto nyingi kama magonjwa na hasa kama hukupata wazo mapema la kumtumikia Mungu . Uliendelea na maisha yako mabaya toka ujana wako, na sasa unajiona kutengwa na jamii, kuhitaji msaada zaidi, kuhitaji mtu wa kukujali.
Watu wenye umri mkubwa hawatakiwi kuwa na stress, huzuni. kama wangekuwa wamejiandaa mapema , wangeweza kukua wakiwa na furaha badala ya kuhangaika na mambo magumu.
Lakini hutaweza kuwa na uhuru wa akili. kwa sababu akili yako ni chombo ambacho ulitakiwa kutunza, kukifanyia service. Sio njia zingine.
Unawezaje kutunza akili yako isiwaze mambo mabaya, badala yake iwe inawaza mambo mazuri.
Kumbuka kuwa Hakuna umri ambao unaweza kukuzuia kufungua uwezo wa akili yako. Unaweza kuwasha taa yako na ukaanza kuishi vizuri bila ya stress na huzuni nyingi sasa hivi. Kumbuka Imani ni sasa.
No comments