Kuwa Single Sio Laana Wala Ugonjwa , Twende Tuone.

happy-young-woman-single-looking-at-phone-1024x773-1024x773 Kuwa Single Sio Laana Wala Ugonjwa , Twende Tuone.
Kuwa single ni kuwa mkamilifu, lakini watu wengi wanafikiri kuwa ni laana au kukosa bahati. Wanawake na wanaume wengi wanaishi kwa masikitiko wakifikiri kuwa hawana ngekewa ya kupata wenza.
Nataka nikupe mbinu mbalimbali za kukusaidia kufahamu upekee wako wakati ukiwa single. Kumbuka kupoteza muda ni kupoteza maisha. Ukiwa unafikiria kwa nini uko peke yako kama wengine ambao wako wawili wawili, utapoteza muda mwingi . Wekeza muda wako ili uwe na maisha mazuri. Fanya  kazi kwa bidii , usipoteze muda wako kufikiri au kutaka kupata mtu wa kuishi nae kama muda bado haujafika , huwezi kulazimisha.
Mungu aliumba hapo mwanzo watu wawili tofauti,  na huko ndiko kulikotokea mtu kuwa mmoja. Adamu na Eva waliumbwa wakiwa single. soma Mwanzo 2:7 . Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia  pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai.

young-man-smiling-at-phone-1024x683-1024x683 Kuwa Single Sio Laana Wala Ugonjwa , Twende Tuone.
Adamu akapewa majukumu ndani ya Bustani ya Edeni, hakuwahi kupungukiwa wala kuwaza kuwa yuko peke yake. Maisha yalikuwa bomba sana. Mungu yeye ndiye aliyeamua kumuumba Eva ili awe msaidizi, baada ya kuona kila alichokileta mbele ya Adamu hakikufanana na yeye. Kwa hio hilo lilikuwa ni wazo la Mungu. Kumbuka kuwa msaidizi maana yake sio kupungukiwa na kitu au kukosa kitu bali kuna kazi zilizidi kwa Adamu ndio maana ya kuletewa mtu wa kumsaidia.
Kwa hio wewe ambaye uko single usifikiri kuwa ni vibaya. Wakati ukiwa single  ndio muda mzuri wa kujitafuta mwenyewe, ujue upekee wako, wewe ni mzao mteule , ukuhani wa kifalme,Taifa takatifu , mtu wa milki ya Mungu, ili upate kuzitangaza fadhili zake Mungu aliye kutoa gizani na kukuweka katika Nuru  ya ajabu.
Kuwa peke yako sio kuwa mpweke.Yesu alikuwa single,Danieli alikuwa single, Meshaki, shedrak na  abedinego walikuwa single,  Walikuwa ni vijana kama wewe.Timotheo alikuwa single, mtume Paulo alikuwa single, Kuna watoto wa Philipo wa kike walikuwa single , kina Lydia, phoebe, mary, martha,  wote hawa walikuwa single.
Hawa ndio mifano ya watu ambao walikuwa single. kwa nini wewe ujiue kwa kuwa uko single hujapata mwenza au kukataliwa?  Miaka ya kuwa single ni miaka ya kuweka misingi imara kwa ajili ya kuwa na mahusiano mazuri na Mungu, Kuwa na mahusiano mazuri na wewe mwenyewe. Ili baadae uje kuwa na mahusiano mazuri na mtu ambae utaishi naye kama mwenza wako.
Kuwa single utajitambua kuwa wewe ni nani katika uwepo wa Mungu. Itakusaidia kuwa karibu na Mungu, roho yako, mwili wako  na moyo wako.
Mkumbuke Mungu siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo, kabla jua na nuru na mwezi  na nyota  havijatiwa giza. Muhubiri 2:1-2.
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi tumpende. Ufunuo wa Yohana 4:11. Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana , maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote, yohana 15:5.
Msingi pekee wa kukusaidia wewe wakati ukiwa single ni Mungu peke yake.  tafuta mahusiano na Mungu. Mahusiano ya mwanadamu yana mwisho , lakini ya Mungu yanadumu, hata siku moja hayajawahi kushindwa.
Ukweli ni kwamba  ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu, Yatareflect mahusiano yako na watu wengine. jinsi ambavyo utawafanyia watu vizuri, utakuwa unamfanyia Mungu, Mauti na uzima huwa katika uwezo wa  ulimi na wao waupendao watakula matunda yake.  Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema.
Kwa hio kuwa single sio ugonjwa wala  laana , ni wakati wa kujifunza mambo mengi, kujifunza kupika, kufua, kuwapenda watu, kujipenda mwenyewe na kumpenda Mungu. kujifunza kuwa na ujasiri, kuondoa woga.
Jinsi ya Kuwa Karibu na Mungu.
1.Soma neno la Mungu. tafuta maarifa mbalimbali, maarifa sahihi utayapata ndani ya neno la Mungu. Yapo maarifa mengi , lakini sio yote  yanayofaa. kuwa makini  na taarifa unazotafuta.
2.Uwe na silaha za kukulinda, kama kufanya maombi, kufunga kwa kumpenda Mungu sio kwa kutaka kitu au kwa sababu fulani.
3.Tumia Muda wako vizuri. ukomboe wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. tumia akili ipasavyo, usiwe kama mjinga asiyependa kujifunza. kujifunza hakuna mwisho. nenda semina mbalimbali, sikiliza CD mbalimbali za watumishi wa Mungu .
Kanuni iliyo kubwa sana katika maisha ya mwanadamu , itakayokufanikisha wewe mtu uliye Single ni Hii , Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. na ya pili ni hii, mpende jirani yako kama nafsi yako.
Usingle upo mpaka ndani ya ndoa. tutajifunza zaidi tunapoendelea. nimeona kuna watu wengi single na pia wanapita kwenye changamoto nyingi sana.
Somo litakalofuata litahusu faida na hasara za kuwa single.

No comments