Soma Hii Kama Akili Yako Inaumia Na Unahisi Kuboreka
Huenda unajisikia umepotea, na unaona marafiki wako bize hawakukumbuki.
Huenda unahisi hakuna kitu kizuri mbele yako. Unatamani muda uishe haraka uende kulala tena . Huenda unahisi kitu kilichotokea kwako kama ndoto ya mchana. Ni kwa sababu huna kitu cha kufanya.
Ni mtazamo wako unatesa akili yako . jinsi unavyojisikia unavuta hali ile ile ya watu wakuone jinsi ulivyo. Unajihisi kama hakuna kitu kinachowezekana kwako zaidi ya kurudi kulala au kwenda kulewa. Lakini sio kweli. Mara zote kuna kitu cha kufanya.Ni kwa sababu bado uko gizani, Toka gizani nenda kwenye Nuru.
Acha kulalamika kwa sababu zipo kazi mamilioni ambazo unaweza kufanya bila hata ya kumuomba mtu kwa kutumia muda wako tu. Kila siku anza na ratiba yako, unaweza kujifunza kitu ambacho hujawahi kufanya. unaweza kusoma vitabu, unaweza kwenda kwenye semina mbalimbali. Unaweza kwenda baharini kama mahali ulipo kuna bahari. unaweza kutoka na kutembea kwenye Nature. Unaweza kujifunza kupika chakula ambacho hujawahi kupika. Unaweza kuanza mazoezi .Fanya kitu chochote ambacho utakiweza.
Hata kama hujisikii kuvaa hata nguo, hata kama hujisikii hata kusogea, unao uwezo wa kujilazimisha kufanya hivyo. Ondoka kwenye hali hio. Usipoteze siku yako, tengeneza siku yako. Kwa sababu utakapopoteza siku moja ndivyo ambavyo utapoteza siku inayofuata. Usipende kukaa mahali salama kila wakati, unapoteza muda wako. Usipende maisha ya kawaida wakati una uwezo wa kuishi maisha ya juu.
Maisha yako yasiwe na mazoea ya kuamka na kwenda kazini au shuleni na kurudi tena kulala. Pata muda wa kukaa na kufikiri kujiboresha zaidi ya unachokifanya kwa siku nzima. Hisi kama unatembea huku umelala wiki nzima.
Fanya kitu leo, pata kitu ndani ya siku yako, ili ujisikie kuwa mtu bora Duniani, kwamba una faida ya kuwepo hapa. Kwa sababu utatambua kuwa hukutumia muda wako vibaya.
Fanya mazoezi kwa dakika 40 na kuendelea, jibu simu ambazo umekuwa ukizikataa, jibu meseji, Fanya Usafi, Fanya kitu cha upendo kwa mtu mwingine, utaona furaha inakaa kwako. Jipongeze mwenyewe.
Usisubiri Kesho kukamilisha lengo lako. Vitu vikubwa huchukua muda kukamilika, havitokei kwa usiku mmoja. Itakuchukua miaka kadhaa kufika lengo lako. Kama kila kazi zako unaziweka ili ufanye wiki ijayo au mwaka ujao, hutakaa ukamilishe lengo lako.
Huwa ni ngumu sana kusubiri kitu, lakini ni rahisi kukaa muda mrefu bila kufanya kitu, Lakini kumbuka kukaa bila ya kufanya kazi sio afya. Jitoe muhanga kama unataka kufanikiwa maisha yako.
Kama unajipenda, kama unajali furaha yako, Basi weka nguvu kubwa kwenye kitu unachokipenda . Utaipata ndoto yako , hutakuwa mtu wa kulalamika tena. utakuwa umepiga uvivu kwa nguvu zako zote. Fanya kitu leo , Usisubiri kesho.
No comments