Njia Nzuri Ya Kuponya Huzuni Uliyonayo
Ni rahisi kuliko unavyofikiria. Hata kama umepotelewa na mtu uliyempenda sana, Au Umekatishwa tamaa, Huzuni haikubaliki kila mahali. lakini kabla ya kutibu twende tuone huzuni inatokea wapi.
Watu wengi sana wanachanganya huzuni na masikitiko. Masikitiko ni hali iliyopo kila mara unapokosea kitu, unapokosana na rafiki, lakini huzuni ni kupotelewa na mtu ambaye ulimpenda na kuishi naye kwa muda mrefu. Inakuwa vigumu kuamini kama kweli huyo mtu kapotea kabisa.
Ukiwa kwenye hali ya huzuni , utapata hasira, chuki, kuchanganyikiwa na kujihisi kutengwa, kutokula vizuri, kuhisi kupungukiwa na kitu. hali hii huwa haiishi kwa haraka usipoikubali.
Unaweza ukawa unaongea kuwa nahisi huzuni leo. Swali ni kwamba, kwa nini iwe leo? unakataa kitu gani? Kuna tatizo gani limeingia?
Kuna tatizo kwenye ndoa? Kuna tatizo kazini? Au Kuna taarifa gani umeipata?
Tazama vitu vya kawaida kwanza mfano mambo ya kazini kama vile,
Kutokuamini mtu, Mara nyingi umekuwa ukiwekwa nyuma, wengine wanakuwa mbele kuchaguliwa kwenda kazi za nje, Hakuna mtu wa kukuelewa.
Mara nyingi hivi vitu huwa vinajirudia , jaribu kutafuta tatizo ambalo huwa haliondoki.
Kujilaumu
Kujichukia
Unajiona kama huna mvuto, unajiona takataka, unajiona huna nguvu yoyote. mambo kama haya ni sumu inayoharibu nguvu yako na kukufanya ujione huna thamani, hutosheki na kitu .
Kuondokana na Huzuni lazima uchukue hatua kama vile unaingia vitani. hapa lazima ushughulikie yafuatayo.
Mwili. Anza kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki kwa dakika 30-40, itapunguza huzuni, pamoja na mazoezi ya kutembea au kukimbia ambayo yatakupa utulivu wa kichwa chako.
Kama unalala masaa machache au kama unazidisha masaa ya kulala pia inasababisha mtu kuwa na huzuni. Kama una hali hii ya huzuni nakushauri lala masaa 6-7 usiku , jaribu kulala muda huo huo kila siku.
Acha kutumia sukari, pia vyakula ambavyo ukila unajisikia vibaya acha kuvitumia. Chakula chochote ambacho una wasiwasi nacho acha kutumia.
Akili. Kuwa makini na vitu unavyosikiliza kila siku, vitu unavyotazama, unavyoviongea, unachokisoma .
Wekeza muda mwingi katika kujifahamu wewe mwenyewe, acha kujidharau.
Jifunze mambo mengi mazuri, tafuta taarifa nzuri kila siku, jipe changamoto mwenyewe kujifunza kitu kipya kila siku. kitu ambacho unakiona kigumu.
Kiroho. Jifunze kutuliza akili yako kwa kusoma kitabu chako cha imani, tambua mawazo yako , tuliza akili yako kwa kufanya meditation, yoga na kuwa na nidhamu katika mambo mbalimbali kama mitandao ya kijamii. Tv.
Jambo ambalo litakutoa kabisa uondoke kwenye huzuni na litakupa furaha ni kutafuta mahali pa kujitolea kufanya kazi. Hasa kazi za kijamii. kutembelea watoto Yatima, kuwatembelea wajane, wafungwa na kwenda kuwaona wagonjwa na kuwaombea.
Imani. ni mambo ya kiroho. jitahidi kuwa na imani uliyonayo. Amini imani yako.
Uamuzi ni wako. Tiba ya Huzuni unayo wewe mkononi mwako, Pale utakapofahamu chanzo cha huzuni , chukua hatua mara moja kuondoa hilo tatizo.
No comments