Mapenzi Sio Ya Mara Kwa Mara
Nimekuwa nikiandika kuhusu mapenzi , upendo muda mrefu sasa lakini bado sio kitu kinachoeleweka. Ni kitu ambacho hakina fomula.
Hakuna mstari mgumu wala rahisi. Madhari yangu na mitazamo yangu na maelezo yangu mara nyingi yana mabadiliko . Hata sijaweza kuweka katika mfumo mmoja unaoeleweka.
Vitu vingi sana vinavyoelezea nani tunampenda na nani hatuwezi kumpenda na kwa namna gani. vitu vyote hivi vimefungwa kwenye historia , tuko wapi sasa kimaisha, kitu gani hasa cha muhimu kwenye maisha yetu siku za leo, kitu ambacho kinaweza kuwa ni tofauti kubwa kulingana na maisha ya kale .
Lakini ninachokiamini Upendo ni kuuchagua kila siku, mara tunapoamua kupenda, Kiwango na rangi ya huo upendo huwa unabadilika kama vile kinyonga anapofika kila mahali tofauti anabadilika.
Upendo unatokea kwenye mawimbi, unatuosha, unatuzungusha kama mawingu, unatupiga na kututupa kama upepo.
Upendo sio wa mara kwa mara
Unakuja kama hali ya hewa.
Ni kitu gani kinafanya mapenzi yawe mazuri sana. Wakati huo huo upendo unakuwa ni mgumu . Na mara zote unabadilika. wakati mwingine , unapendeza , wakati mwingine mbaya . Mara unapoamua kushirikisha mtu moyo wako, upendo hukua na kumfanya mtu ajisikie anaishi na kupumua vizuri. unakaa ndani yetu , kwa udanganyifu na kwa kikomo. na rangi inabaki kuwa kama isiyoeleweka . Mapenzi yasio mazuri ni mapenzi yanayokaa ndani ya box.. lakini huchukua muda mrefu kukua na kukomaa na kuboreka kuliko mwanzo. miaka mingi.
Kwa Hio Kwa Wakati Huu Tutajuaje? kama upendo huu ni upendo wa kweli wakati tunapoujenga ?
Nimejifunza kwamba Mapenzi huja baada ya muda
Muda ambao mnapika pamoja na kutazamana machoni na kutabasamu kwa pamoja
Muda ambao mnanong’ona masikioni kwa furaha na kuhisi furaha
Muda ambao utakuwa unamtazama mwenzako akiwa amelala na kutambua uzuri wake
Muda ambao baada ya kukorofishana na kupishana kwa maneno mengi lakini bado mnarudi kuwa pamoja
Muda ambao kila mtu atafahamu harufu ya mwenzake
Muda ambao utaanza kujitanguliza wewe badala ya mwenza wako
Muda amabo hutamani kwenda kwingine bali kwa mwenza wako peke yake
Muda amabao utamuona akicheza na watoto na kusahau kama yeye ni mtu mzima.
Muda Ambao utalala kifuani mwake na kutoa mate ya usingizi , lakini unaona ni sawa, unaamua kumkumbatia.
Muda ambao utatamani ungemuona wakati ambao alikuwa kijana.
Muda amabo mtatazamana wote na kuona jinsi gani mmepita changamoto nyingi, bado mkaamua kubaki pamoja.
Hivi ndivyo tunavyojua kuwa upendo upo, kwa kukumbuka zile nyakati na kujikuta tupo pamoja.
Na huu unapatikana tu unapokuwa muwazi, mtu wa kusamehe na kubaki kwenye njia sahihi.
Nimeandika nyakati kwa sababu ni kitu amabacho kinapuuziwa. tunapenda vitu vya haraka na hatuvioni. mara nyingi tunaangalia wakati ujao lakini hatupati, tunapokosa, tunafanya maamuzi ya kujilaumu.
Kwa hio fahamu kwamba Upendo sio wa mara kwa mara , hauna uhakika .Upendo ni mwendelezo na ni kitu cha kugunduliwa mara kwa mara kwa kupitia hizi nyakati ndipo utajua kuwa upo.
Kwa kadri nyakati zinapoendelea kuja
Huwezi kuulazimisha
Unaachia nafasi kwa kila mtu kujifunza
Na kama utasimama huenda wewe ndio utakuwa umesimamisha au mwenza wako.
Na ule upendo uliokuwa unakuwa, haukui tena
Utakuwa upo ndani ya chupa sasa
Huenda huo ni woga dhahiri unakupata.
Usihofu hakuna kisichowezekana . Ukimtumainia Mungu.
No comments