KAMA HAUTUMII VYAKULA HIVI, NGUVU ZA KIUME UTAZISIKIA REDIONI
Nguvu za kiume ni nini?
Huu ni uwezo wa mwanaume kuweza kusimamisha uume wake na kuhimili mda mrefu kwenye tendo la ndoa bila kuchoka kirahisi.
Waswahili wanasema ni “uwezo wa gari kupiga starter lenyewe bila kusukumwa”
Utafiti unaonyesha kati ya wanaume watatu, mmoja ana tatizo la nguvu za kiume kitu ambacho kinaonekana kitakua zaidi siku zijazo.
kwa fursa hii watu wengi wamejiita waganga na kuuza dawa nyingi za uongo wakidai zinaongeza nguvu za kiume ili kujipatia fedha kitapeli.
nakushauri wewe msomaji usiangukie kwenye mtego huo.
Kuna sababu kadhaa ambazo zinasababaisha kupungua kwa nguvu hizo lakini hii sio maada yangu kwa leo ila ntaziongelea session zijazo.
Vifuatavyo ni vyakula ambavyo vinaweza kukurudishia nguvu zako za kiume kwa asilimia mia moja{100%].
· Banana {ndizi mbivu}
Haya ni matunda ambayo yanapatikana kwa wingi nchini kwetu na kwa bei nzuri, enzyme muhimu iliopo kwenye ndizi kwa jina la kitaalamu bromelain huongeza stamina na hamu ya tendo la ndoa.
Pia vitamin B, ambayo hupatikana kwenye tunda hilo huongeza nguvu za mwili.
· Garlic {kitunguu swaumu}:
Kitunguu hichi ni hutumika sana kwenye mapishi ya kiafrika hasa upikaji wa pilau, lakini hufanya kazi vizuri kikiliwa kibichi.
Kitunguu hichi hufanya kazi ya kuongeza mmiminiko wa damu kwa wingi kwenye uume na kufanya mwanaume kustahimili vizuri kwenye tendo hilo.
· Pea nut{karanga}:
Karanga ni moja ya vyanzo vikubwa vya amino acid ambayo kitaalamu inaitwa L-arginine ambayo hufanya kazi ya kulegeza mishipa ya damu ya uume na kuruhusu damu kuingia kwa wingi hivyo kuupa uume nguvu maradufu.
· Chocolate:
Ni chakula kinachopatikana kwa wingi madukani, ambacho kitaalamu kina kemikali zinazoitwa phenylethylamine na alkaloid, ambazo huongeza nguvu na stamina wakati wa tendo la ndoa.
· Blue berries:
Haya ni aina ya matunda ambayo hayapatikani kirahisi nchini kwetu ila yanalimwa san amerika ya kaskazini na hupatikana mara chache mijini kwenye supermarket kubwa kubwa. Matunda haya hufanya kazi kwa kupunguza lehemu{cholesterol} kwenye mishipa ya damu na kufanya damu kupita kwa wingi kwenye mishipa hiyo na kuufanya uume usimame kwa nguvu na kwa mda mrefu.
MWISHO: ni kiasi kidogo tu kinahitajika kwa siku, kwa vyakula nilivyotaja hapo juu.
hivyo sio busara kula vyakula hivyo kwa wingi na kuacha kwa wiki moja.
Ni vizuri ukala kiasi kidogo kwa mda mrefu ili upate matokeo mazuri.
No comments