UFAHAMU UGONJWA WA CHUNUSI NA MATIBABU YAKE.{acne vulgaris}

       


                             
chunusi ni nini?
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi.

chanzo ni nini?
hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote.

matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibababu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.


matibabu ya chakula..
 ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
 epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.                                                                                                                                                                                                             
 epuka nyama za wanyama wote unazozifahamu, viungo vya bonga i.e pilipili, na stimulants ie kahawa.nb: unaweza kula samaki kama huwezi kuvumilia bila kula nyama.
pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana  pia kula kwa wingi karoti mbichi kwasababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.

matibabu ya  kimwili.
 acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku.
shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jashoo kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.                                                                                                                                       
 matibabu ya dawa
kuna dawa zinasaidia kuondoa chunusi i.e antibiotiki kama doxcycline, vidonge vya vitamini A na vidonge vya hormone kwa wanawake mfano eotrogen, persol tube na kadhalika.

 mwisho:
 watu wengi hawaponi chunusi kwasababu ya kupenda  kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa}, ni vizuri kuchanganya njia zote hapo juu kwa matokeo mazuri na inaposhindikana ni vizuri kumuona daktari bingwa wa ngozi kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

No comments