MAANA YA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME?

Unapopungua nguvu za kiume, kama nilivyosema hapo awali, ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana. Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi; au

2. Uume kusimama kwa uregevu; au

3. Kuwahi kufika kileleni; au

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; au

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo; au

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji; au

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Ndugu msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Tukichukulia mfano wa kiwanda, ni kwamba ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili, na siyo kukurupuka kubugia dawa tu.

Lakini, nini kinachosababisha viungo hivyo vishindwe kufanya kazi?
Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia). 

Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.

Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya side effects za madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid. 

Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.

Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo ugonjwa bado uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Yani unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu au vitu havifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua haraka  TAHADHARI kabla ya HATARI!

No comments