Mapenzi Mazuri Ni Ya Wakati Uliopo
Tunatumia muda mwingi sana kutaka kujua kama mtu tunayempenda kama na yeye anatupenda, hio inatufanya kusahau jinsi ya kufurahia mapenzi jinsi yalivyo, wakati uliopo.
Kwa wakati ambao upendo hutokea, tunatumia muda mwingi kushangaa jinsi gani umetokea, jinsi gani tutaweza kudumisha mapenzi, yawe bora na ya kudumu. Ukweli ni kwamba kila mtu ana mtu wake ndio maana utakuta ndoa zina shida nyingi kwa sababu ya kulazimisha ubavu ufiti sehemu ambayo sio yake.. Lakini watu wamekuwa wakipewa maneno matamu ya kuwafanya waendelee kuvumilia huku wanateseka. mihemko ya mwili na kuangalia sana movies.
Njia pekee ya kupenda kweli ni kumpenda mtu wakati uliopo, wakati sahihi, wakati ambao mwanaume tayari ana kazi yake mwenyewe . Wakati ambao mwanaume amejaza masaa yake 24, na mwanamke ambaye amejaza masaa yake 24. utapata kiss nzuri, mahali pa utulivu, na kusahau uchovu wote wa siku nzima. Mapenzi ni chumba chenye utulivu, mkiwa wawili, mkiwa mnalengo moja kwa wakati uliopo.
Huu ndio upendo wa kweli unapotokea. Hii ndio inaonyesha upendo wa kudumu. Sio aina ya mapenzi ya kwenye movies, sio upendo unaokauka, sio wa kutamkiana kwa maneno. Upendo, upendo wa kweli una hisia zenye usalama, hazina haraka. Ni ukimya wa chumba cha hospitalini unapotambua kuwa mtu unayempenda yuko salama. Ni hali ya kujisikia amani kila unapokuwa na mpenzi wako, ni mahali unapojisikia uko nyumbani, umefika home. Unapokumbatiwa na kukumbatia, unaposikia lile joto zuri moyoni na mwilini. Huo ndio upendo.
Jitathimini mwenyewe mahali hapo. Wakati uliopo kuliko kuanza kufikiria tofauti. Nakuhakikishia hutashindwa katika mahusiano.
Upendo ni kitu kigumu. Ni tunda ambalo unakula lote hutupi kitu chochote.
Furahia mapenzi kwa wakati uliopo.
No comments