Sio kwa  namna ambavyo mnakiss
Sio kuhisi utamu kama asali
Sio kujihisi kama uko hewani wakati uko chini kawaida
Au kwa namna ambavyo mnafurahi
Hata kama mnafahamiana kwa miaka mingi kiasi gani
Wala sio kwa miezi michache baada ya kufahamiana.
Sio kwa namna ambavyo macho yako yanavyotazama macho yangu
Kama vile unaona ramani unaichora kichwani mwako
Sio kwa namna ambayo utanichukua nyumbani kwako
Wala sio kwa namna ambayo utanifanya niwe wako maishani
Sio kwa njia ya sex kama wengine wanavyofikiria
Ni njia rahisi tu. Njia ambayo ulitumia kunifahamu kabla  sijaamua au kukubali kufahamika kwako.
young-african-american-couple-remote-footage-000826510_prevstill-1024x576 Wakati Mwingine Mapenzi Ni Rahisi
Ni jinsi ambavyo umenikubali jinsi nilivyo
Ni mapenzi ambayo hayahesabu kitu chochote.
Ni furaha na amani  iliopo kwako na kwangu.
Ni Mungu tu.