OGOPA SANA: Ukiona Mwanamke Anafanya Mambo Haya ,Ujue Hajakomaa
Ni mwanamke aliyekomaa au bado mchanga?
Hapa kuna baadhi ya dalili ambazo zitakuonyesha kuwa huyo bado hajawa mwanamke.
1.Anaigiza kimalikia
Kuigiza kama malikia ni aina ya uchanga ambao mara nyingi sio hali yake ya kawaida. Hajielewi bado. Haijalishi ana ukubwa gani au udogo gani, Kila unapokuwa naye huwezi kumuelewa, ana mambo ya kuiga .
2. Hana Ujasiri
Ni kweli kwamba wote huwa tunakosa ujasiri wakati kwa wakati, lakini msichana huyu anahitaji mtu amuhakikishie kila kitu, hawezi kujiamini mwenyewe, anahitaji maoni yako kabla hajaamua kitu.
3.Hawezi kusimama Mbele ya Watu.
Ni mwoga,Hawezi kuongea mbele za watu wale kusimama na kupita mbele za watu wengine kwa kuogopa kusemwa au kufikiriwa vibaya na watu.
4.Hisia zake zinatawala maisha yake.
Anaachia hisia zote za woga, wasiwasi, mashaka yamtawale. ilimradi anapelekeshwa tu. bila ya kufikiria matokeo yake au matatizo yake. hajajifunza jinsi ya kukabiliana na hisia ndani yake.
5.Anamweka mwanamme kama ndio Ulimwengu wake
Wakati msichana akiwa single, kazi yake kubwa ni kutafuta mwanamme yeye mwenyewe. akimpata ni kama mwezi wake. lakini mwanamke aliekomaa huwa na maisha yake na anajifahamu vema hata akiwa na mwanamme kwake ni kawaida.
6.Ni mtu wa tahadhari
Wasichana hutafuta usikivu, lakini wanawake hutafuta heshima.
7.Anajali sana kuhusu watu wanafikiria nini na kusema nini.
Anaishi kutokana na kuona jinsi gani anakubalika. anataka kuonekana mzuri na mtu wa kupendwa na atafanya kila njia awe hivyo. Waliokomaa wao hubaki katika ukweli wa uhalisia wao . hawajali nani anapenda au hapendi jinsi alivyo.
8.Anaweza kuishi hata na mvulana mbaya kwake ni sawa
Hata kama mwanamme hampendi, lakini atajitahidi kulazimisha, atatumia kila mbinu. wakati mwingine anaona kabisa huyo mtu ni tatizo lakini hawezi kufikiria. anachowaza ni kwamba nitampata tu.. Amini kwamba mwanamke aliyekomaa kiakili hafikirii na wala hana muda wa kupoteza katika hayo.
9.Anakuwa na Wivu Na Wanawake Wengine
Kila anapoona mwanamke yupo na mwanamme wake , wasiwasi unamjaa. Anaanza kujilinganisha kwa sababu hajiamini .hajikubali , hajipendi na wala hajijali. Lakini mwanamke mwenye kujua kujipenda, kujijali , kujikubali na kujiheshimu hana wasiwasi huo .Anamwacha mume wake huru na yeye anakuwa huru kuongea na mtu yeyote.


No comments