Usidate Naye Kwa Sababu Tu Ya Upweke Ulionao.

1501cd0eca4d6d8faeade48f02f9eb14-black-guys-black-men Usidate Naye Kwa Sababu Tu Ya Upweke Ulionao.
Usidate naye kwa sababu ya upweke wako. Usitumie muda mwingi wa kuongea naye sehemu  kwa kujilazimisha. Usikubali kutoka naye. Usiseme ndio Kwa sababu ya kutaka kuondoa hamu ulionayo.
Usidate naye kwa sababu umekosa meseji za asubuhi na za  kuambiwa ulale salama babe. Anaweza awepo hapo lakini asikufurahishe kitu.  Usidate naye kama huridhiki naye, utapata shida. Atakuwepo na wewe lakini utakuwa bado unajisikia mpweke kwa sababu sio unayemtaka.
Usidate naye kwa kuogopa kutokupata mwingine.Kwa sababu my dear, yupo  mtu mahali kwa ajili yako.  Ni kwa sababu hujui kama yupo sehemu. Kwa hio usipoteze muda na mtu ambaye huna hisia naye, mtu ambaye huwezi kufurahia uwepo wake kila unapomuona akiwepo upande wako.
Na kitu cha muhimu zaidi usitulie. Usijifanye unafurahishwa na utani wake . Usifanye kitu ambacho hutaki kukifanya kwa sababu amekuambia ukifanye. Usijifanye kuwa anakufurahisha, wakati unaelewa kabisa hafanyi kitu. Usishushe viwango vyako au kujilazimisha  hisia ambazo hazipo kwako.  kwa sababu utakapokuwa na mtu sahihi mahali popote hutaweza kutumia nguvu– wakati wa mazungumzo. Ucheshi,  meseji za asubuhi  na za usiku mwema na  goodnight kisses  zisikutishe unamaliza nguvu zako bure.
Kwa hio usiwe na mtu ambaye hafanyi Ulimwengu wako uwe ni sehemu yako  ya furaha. Usiwe na mtu ambaye hakuwezeshi kutabasamu anaposema jina lake tu. Usiwe na mtu ambaye hayupo akilini mwako kila wakati, ambaye hawezi hata kukupigia simu  hata wakati ambao hukufikiria.
Usidate naye kwa sababu tu unapunguza upweke wako, kwa sababu kama ukifanya hivyo,  unaweza ukamkosa  mtu ambaye angeweza kujaza  kila kitu ambacho ulikitaka.
Zaidi ya yote kaa chini kwanza na ujaribu kutafuta taarifa kamili kabla hujaamua kujiingiza kwenye aina yeyote ya mahusiano. Usije ukalipia gharama  kubwa baadae. Uwe na subira, na usubiri  process ya Mungu.
Jitahidi ukue kiakili, kiroho na  uwe mwenye afya kimwili.
Kama umefaidika na makala hii washirikishe wengi wajifunze.
kisha  Subscribe kupata kilicho bora  kila mara.

No comments