Aina Ya Upendo Unaohitaji Kusubiri Uje Kwako
Hii ndio aina ya upendo ambao unahitaji kusubiri . Sio aibu au Kusita. Sio kitu ambacho utafikiria kukilazimisha. Utajisikia kuwepo nyumbani kwa usalama.
Upendo huu unaotaka kushikilia ni wa nadra.Upendo huu huja mara moja . hauna vipingamizi. Lakini kuwa mvumilivu. Kuwa na tumaini hilo. Na usiache kuamini .
Upendo huu unaousubiri ni wa ufahamu na uangalifu mzuri. Ni wenye heshima na uaminifu. Umejawa na utele wote wa kuishi kwa furaha na amani. Utakupigania wakati ambao hujiwezi na huna la kufanya. Utakuwa ndio makazi yako. Ulinzi wako. Ndio nusu yako uliyopungukiwa.
Aina ya Upendo unaohitaji kusubiri ni aina ambayo inastahili kusubiri kwa muda wa kutosha na kipindi hicho kiwe cha kujiweka sawa. katika kujiimarisha kiakili, kimwili na kiroho. Niamini mimi.
Kwa sababu upendo huu utakuwa ni wenye nguvu ya kipekee, na utakuwa ni laini . Utajisikia salama na kupata joto zuri , kama mtoto anayerudi kukumbatiwa mikononi mwa mama yake. Utajisikia kupumua vizuri bila matatizo na utapendwa na kuthaminiwa.
Upendo unaohitaji kusubiri sio wa kutazama aina ya kazi au pesa alizonazo mtu. itakuwa ni kuhusu mioyo ya watu wawili imekutana pamoja kwa wakati sahihi. Mtajengana wote pamoja na wakati huo ukiendelea kujijenga mwenyewe binafsi.
Upendo unaosubiri hautakuangusha. Unaweza usielewe wakati kwa wakati upepo unapopita, lakini hautaweza kuvunja .
Upendo unaosubiri utakuwa wa kudumu. Utadumu na utaboresha afya ya mioyo yenu . Upendo huu utakupenda wakati wote , iwe kuna mabaya au mazuri. Utakushikilia mpaka utakapo kuwa na wakati mzuri wa kutulia tena. Upendo huu ni ule ambao hutaacha kupigania furaha iwepo kwenu.
Upendo unaosubiri ni wa Nadra. Ndio. Lakini utatokea kwako.Unachotakiwa ni kuwa mvumilivu. Usitulie mahali ambapo sio kiwango chako. Unastahili kupata huo Upendo hapa Ulimwenguni.
Ipo siku utatazama nyuma na kutambua kuwa miaka yote uliyosubiri umestahili kupata upendo huo na zaidi. kwa sababu utatazama muda uliopita na kutabasamu. Kwa kuwa utakuwa umekamilika.
Kwa hio usitulie kwa kitu kidogo au kujiwekea alama ya ulizo. Usijifanyie hivyo, Usidhulumu moyo wako na kujiona sio wa muhimu na kuhisi hustahili kupata unachokitamani kukipata maishani mwako. Usitulie kwa kidogo au kwa nusu hio hata kidogo.
Moyo wako unastahili hiki. Unastahili kupata Upendo mkubwa ambao kila mtu anapenda kuupata. Lakini nakuambia wewe kuwa Unastahili. Kamwe usfikiri kuwa huwezi. Na kamwe usiache kuamini.
Utaupata Upendo huo Hivi karibuni. Utaupata.
Kama umependa makala hii washirikishe wengi
Na Mungu Akubariki kwa kufanya hivyo.


No comments