Vitu Muhimu Katika Mawasiliano
Sifa ambazo zinasaidia watu kuwa na umoja wa ndani zaidi.
Mara nyingi wanandoa wanalalamika kuhusu kuwa na matatizo katika mawasiliano. Lakini kama tukiangalia ndani zaidi , Kuna misingi yenye sifa ambayo ni muhimu kwa ajili kujenga afya ya mahusiano , Urafiki kwenye mahusiano. Wakati unapotambua na kufanyia kazi, tunakuwa kwenye nafasi ya kuwa na ukamilifu. .
Kukumbuka.
Uwezo wetu wa kuwasiliana unabakia kwenye uwezo wa kuwa makini wa kitu tunachojisikia ndani. Inachukua muda wa kukumbuka kipi hasa ambacho tumekifanya.
Kurudisha umakini ndani , tunaweza kutambua kuwa wakati huu nasikitikia kitu fulani, kuogopa, au kusikia upweke. Au tungeweza kutambua aibu ambayo mmoja amefanya na kutuletea kuchanganyikiwa. Tunaweza kuwa tunasikia hasira kwa sababu ya kufanyiwa kinyume na tulivyotarajia.
Changamoto iliopo kwenye mawasiliano ni pale tunapomshutumu mtu mwingine na kusahau upande wetu kuwa hatukufanya chochote zaidi ya kuhukumu mtu mwingine. Mfano kusubiri kupigiwa simu au kutumiwa ujumbe na mwenza, Kwa nini usipige wewe kama yeye hajapiga au kutuma ujumbe.
Tunatawaliwa na matukio ya nje . Tunajaribu kubadilisha mtu mwingine badala ya kujibadilisha wenyewe. Njia nzuri ni kubadilika mtu binafsi badala ya kutaka kumbadilisha mwingine.
Mara nyingi majibu yanakuwa sio mazuri. hayapendezi . Utakuta mtu anaongea vizuri na mtu mwingine kwenye simu , lakini akiwa anaongea na mwenza wake utaona sura yake inavyobadilika. Maneno yote ni ya kulaumu na kulalamika na anaamini kuwa anawasiliana naye vizuri. Badilika kama uko hivyo. mwenza wako ni mtu ambaye unatakiwa uongee naye vizuri kuliko mtu yeyote.
Ukweli wako wa ndani mara nyingi hauko vizuri . muda wote wewe ni kushambulia , kuhamaki, kulaumu, na kujilinda upande wako. Kubali kufahamu kuwa hizo hisia sio nzuri. Unahitaji kubadilika kama unahitaji kupata mawasiliano mazuri. Anza kujichunguza wewe ndani yako , upo upendo? Umefanya kama unavyotaka ufanyiwe? Umejali kama unavyotaka mtu akujali wewe?
Kuita UJasiri
Tunaweza kutambua thamani na kutunza utulivu na kumbukumbu na kuelewa uzoefu wetu. Lakini bila ya ujasiri , tunakuwa watu wa kujilinda nafsi zetu tu , na kujilinda kutoka kwenye maumivu yenye aibu.
Ujasiri maana yake ni kuwepo kwenye uzoefu zaidi kuliko jinsi ambavyo tunalalamika. ujasiri unatokana na moyo, Maono yako yanatokana na kutazama ndani ya moyo wako. ambaye hutazama nje ya ndoto. ambaye hutazama ndani ya uamusho. tunaishi kwa ujasiri kama tunavyoishi kwa moyo na bila ya woga.
Ujasiri ni kufahamu kuwa haijalishi ni wakati gani, uwe ni mzuri au ni mbaya ni lazima uzoefu wetu uwajibike. hakuna aibu , tunaweza kuishi kwa kufahamiana matendo yetu kwa uzuri, bila ya kuwa watu wa hasira. tunaweza kutulia na kuvuta pumzi na kutambua kitu ambacho tunajisikia muda huo na tunaweza kuwa na ujsiri wa kukutana na uzoefu bila ya kuhamaki.
Ni vizuri kutafuta ujasiri kuliko kulaumu na kulalamika tunapokuwa na mawasiliano kati yetu. Urafiki wa karibu una maana ya kuona kila mtu ndani ya ulimwengu wako. karibisha mtu ndani yako , mshirikishe ndani ya maisha yako na umwamini , hapo mtakuwa watu wa furaha na hakuna wa kumlaumu mwingine.
Natumaini umepata kitu

No comments