Onyesha Umuhimu Wake Kwako
Kila msichana ana ndoto ya kuwepo kwenye mahusiano sahihi, Ni kama vile kwenye movies.Wana matumaini yote na kusubiri bila ya kuwa na mapenzi na mtu mwingine , nia yao ni kupata mtu sahihi.
Lakini hakuna kitu kama sahihi. Msichana hategemei wewe upeleke mwezi na nyota ili kumhakikishia kuwa unampenda. Wanachokitaka ni kupata mtu anayejali.
Wasichana sio tu kwamba wanataka mwanaume mwenye kujazia na mwenye uso mzuri. Wanataka kiini sio form. Wanataka mtu ambaye wataweza kuongea kuhusu malengo yao na ndoto zao mpaka saa tisa asubuhi. Wanataka mtu ambaye wataweza kuongea naye kuhusu ndoto mbaya walizoota, na mtu wa kuwaambia kwamba uko sahihi ni ndoto tu, hakuna shida.
Hawapendi hayo maneno ya uongo ya kudanganya na ahadi za uongo. Usiwafanye washikilie kitu ambacho huna uhakika nacho. Maneno ni bure kama vitendo hakuna. Hata nguvu kidogo tu inaweza kuwaletea tabasamu kwenye nyuso zao.
Wasichana hawapendi viatu vyenye majina makubwa, mabegi yenye majina ya kusifika. Sio wasichana wote wako hivyo. Naongelea wasichana wenye msimamo. wanataka kitu halisi. Kitu ambacho wanaweza kuonyesha ulimwengu na kujivunia nacho.
Hawataki kuwa nyara. Wanataka kupendwa jinsi walivyo, sio kwa tofauti. Sio kitu ambacho utakionyesha tu kwa wengine.
Wanataka kusikilizwa na kusikika pia. Wanataka ukweli. Wanataka uhalisia, sio kumfanya aamini. Hawataki vitu ambavyo utafikiria kuwa ndio kuonyesha upendo wako.
Wanataka uonyeshe ni kiasi gani unajali. Wanataka tu kukupenda, na kupendwa. Hata kama itakuwa kila siku. ilimradi awe na uhakika kuwa ni kiasi gani unaona umuhimu wake kwako.
Hawapendi kuuliza kupita kiasi. Haigharimu kitu kikubwa cha kumfanya akae kwako. Anakutaka wewe tu na upendo wako.
Umewahi kufikiria kitu kama hiki?
Toa maoni yako kusaidia wengine.

No comments