Urafiki Ndani Ya Mahusiano
Sababu kubwa inayoleta matatizo kwenye mahusiano —na huenda ikawa ni kubwa zaidi—Ni Hukumu. Ikiwa na maana ya mtu kujihukumu mwenyewe na kuwahukumu wengine.
Kujihukumu ni hali ya kujitenga. Tunapojihumuku wenyewe, Ni rahisi kuwahukumu wengine. na ni kinyume chake.
Mara nyingi tunapojihukumu na kuwahukumu wengine Tunaamini kuwa tunasababisha mabadiliko, lakini imeonekana kwamba hali hii inaleta wasiwasi, huzuni, kujilaumu, au kuona aibu. hutakuwa na utendaji ulio bora hasa katika furaha na amani .
Kwa Hio Kitu Gani Kinatokea Kati Yako Wewe Na Mwenza Wako ,mtoto, rafiki, Mfanyakazi mwenzako wakati unapojihukumu na kuwahukumu wao?
Unapokuwa na tabia ya kujihukumu , unakuwa unahisi kuwa watu wanakuhumu wewe, Na unapojihukumu unakosa usalama. Ukweli ni kwamba Hakuna kitu kizuri kinaweza kufanyika kama utajihukumu na kuwahukumu wengine.
mapenzi Tabia Inayoua Urafiki Ndani Ya Mahusiano
Hata unapoachia mawazo yako mabaya , yataharibu au kuathiri frequency zako. Mahali pa ndani ambacho unafanyia kazi ya kujilaumu na kuwalaumu wengine. Unapojilaumu au kuwalaumu wengine frequency yako inashuka chini . Huwezi kujiunganisha na wengine kama moyo wako umeufunga
Utawezaje Kuzuia Hali HII?
Kama unataka kujiunganisha na upendo ndani ya mahusiano, Unahitaji kuanza kutambua mawazo yako. huwezi kuacha mpaka hapo utakapotambua kuwa kuna kitu tofauti. Sio kitu cha kawaida kubeba mawazo ya kujihukumu na kuwahukumu wengine.
Wasiwasi mwingi unatokana na kujihukumu na kuwahukumu wengine. Mimi nilianza kutambua na kuanza kufanyia kazi mawazo yangu na nikaanza kuacha hali ya kujihukumu na kuwahukumu wengine. Na sasa maisha yangu yamebadilika kabisa.
Anza kubadilisha hali ya kujihukumu kwa kujikubali na kuwakubali wengine, Kuwa na huruma na kusamehe. Unapojikubali na kuwakubali wengine, kujisamehe na kuwasamehe wengine itakufanya uwe mwanadamu. Frequency zako zitakuwa juu na moyo wako utakuwa wazi. kwa mtindo huu utajisikia rahisi kujipenda na kuwapenda wengine.
Hii Sio Tu Kujiunganisha Na Wengine , Ni kujipenda kabisa na kujikubali.
Kwa hio Ondoa Kujihukumu kwa Kujikubali. Kuwa na huruma, kusamehe na kujijali. Utaanza kuona upendo na ulinzi ukiwepo pamoja na wewe.
Huwezi kupata ulinzi endapo umefunga moyo wako, na kujihukumu kunafunga moyo wako. Kila mara kumbuka kuwa Mungu anakupenda. Anakujali, amekukubali jinsi ulivyo. Anakulinda. Kwa nini unaogopa. Unafikiria kuwa uko peke yako.
Nafikiri unaweza sasa kuona hiki kitu kimoja kikubwa kinachobadilisha katika kufikiria kwako kina athari kubwa kwenye maisha ya kila mtu na katika mahusiano yote.
Nakutia moyo ,Anza sasa kutambua kuwa hukumu inafanya kitu gani katika maisha na mahusiano yako na uanze kubadilisha haya kwa huruma , kujikubali na kusamehe.
Toa maoni yako kusaidia wengine.

No comments