Mambo 10 Yanayoboresha Mahusiano Yako

help-your-spouse-through-hard-time-2-1024x682 Mambo 10 Yanayoboresha Mahusiano Yako
love
Sifikirii kuwa kuna mtu yeyote anaweza kuuliza kuhusu jinsi gani ya kuwa na mahusiano mabaya  yenye matatizo kila kona.
Sio tu mahusiano mazuri na yenye afya. Nadhani tunacomplicate mpangilio mzima wa  mahusiano mazuri kwa kukazania zaidi  mambo ya kijinsia na ya kijamii.
Moja ya kipengele cha mafanikio ya mahusiano ni watu wote kuwa katika usawa wa  thamani zao. Kama hukubaliani katika usawa, Unafikiri utakubalianaje?  haitawezekana .
Kama unataka mahusiano yadumu kwa kipindi chote cha maisha yako na kuwa na furaha , wote muwe serious katika mambo ya muhimu ambayo nitayasema hapa chini.
1.Unaamini kwamba mwenza wako na wewe mko sawa
Wote muwe na mtazamo mmoja na kutambua haki ya kila mtu.kama hamtakubaliana katika usawa, mtawezaje kuzungumzia hisia zenu, mihemko yenu,mawazo yenu au kitu kingine chochote?
Mahitaji yenu yanatakiwa yaeleweke kila upande kwa usawa kwa sababu hakuna aliye bora kuliko mwenzake.
2.Unatoa na kupokea
Mara nyingi matatizo mengi hutokea kwenye mahusiano kwa sababu , mmoja anakuwa mtoaji kuliko mwingine.  kuna anayejua kupokea tu bila kutoa. Lazima kuwepo usawa. ukitoa ni lazima kupokea. ukipokea ni lazima kutoa. tena ni vizuri kama utajua kutoa kuliko  kupokea.
3.Hakuna kutawaliwa na mwingine.
Hakuna haja ya kujaribu kumtawala mwenza wako. Wenza wanatakiwa kuheshimiana,  Na kukubali mawazo ya kila mtu na kuyafanyia kazi. Kuzungumzia mawazo yao kwa kuheshimiana hata kama ni ya utofauti mkubwa. Hakuna haja ya kujaribu kutawala akili ya mtu  au mawazo ya mtu. Hakuhitaji kusafisha ubongo hapa.
Ugomvi, matusi na kusemana vibaya sio sehemu ya  mahusiano yenu.
4.Kumkubali mwenza jinsi alivyo.
Wote tuna madhaifu, hakuna aliyekamilika , kitu cha muhimu ni katika kufanyia kazi  mambo ili yaendelee vizuri.  kujifunza kupenda  madhaifu ya mwenza wako.
Kuwepo na mtazamo mzuri.  usimtazame mwenza wako kwa mtazamo mbaya, jitahidi kumuelewa.
5.Usijaribu kumbadilisha mwenza wako.
Kila mtu amkubali mwenzake jinsi alivyo. usijaribu kutaka kumbadilisha mtu, labda kama ataamua kubadilika yeye mwenyewe. Mkubali katika hali zote, positives na negatives alizokuja nazo.
Haikubaliwi kumwambia mwenza wako kuwa usivae mashati ya kubana au makubwa. Au kwa nini hukati hizo nywele zako. Kwa mtindo huo mahusiano hayataweza kufanya kazi nzuri.
6.Kila mmoja ana mwamini mwenzake.
Sentensi hii inaweza kuonekana ngumu kidogo. lakini  sio kwa sababu ya kufikiria vipi kama kitu fulani kitatokea na kinamfanya mtu akumbuke kitu fulani? Kama utamkamata  mwenza kwenye uzinzi, kuna kuaminiana tena?
Hapa inatakiwa kuwa na imani na matumaini. Kusamehe na kusahau. japo kovu huwa halitoki endapo umeuguza kidonda na kikapona. Lakini pia kumbuka kovu likipona huwa haliumi , linakuwa kama historia.
7.Kusaidiana kukua kiroho, kimwili, na kiakili.
Kwa sababu mmekuwa kitu kimoja , ni vizuri kupeana moyo, kusaidiana, kuleana, kupata uzoefu  wa maisha pamoja.Kukumbatia mabadiliko ya kukua kwenu.
8.Kuwajibika kila mtu
Wote mnakuwa pamoja katika mambo yote . muwe huru katika kuongea, kutoa maoni yenu, kufanya kazi pamoja.
kila mtu athamini mawazo ya mwenza wake, hisia za mwenzake na maoni ya mwenzake, imani zenu, mkubaliane .
9.Kila mtu alete Ubora Kwa mwenzake.
Kwa kawaida hutakubali mtu akuletee mambo mabaya, mtu wa kukurudisha nyuma,  Bali mtakuwa watu wa kupongezana kwa upekee wenu na hio haitokani na mwonekano.
Wote mko kwenye level moja  na wote ni watu wazuri.
10.Mtakuwa na uzoefu wa urafiki wa kimapenzi
Hii inahusisha vyote kimwili na kiakili. Sio kuhusu sex tu. ni kuhusu hisia zenye nguvu mlizonazo na kuonekana kupitia kipengele cha  urafiki wenu wa kimapenzi. Ni kuhusu watu wawili kupitia vitu vyote kimwili na kiakili.
Ili kupata uzoefu  wa mahusiano yenye afya nzuri na yenye furaha, hivi vitu 10 ni vya muhimu  katika kufanikisha mahusiano ya kudumu.
Unaweza kutoa maoni yako hapa ili kuwasaidia wengine.

No comments