SAYANSI YA MAPENZI;JINSI MAPENZI YANAVOTOKEA KISAYANSI.
Professor Arthur Arun amekua akitafiti kwanini watu huzama katika mapenzi,akachukua baadhi ya watu na kuwaambia wafanye mambo matatu(3) ambayo yameorodheshwa hapo chini, na kugundua kwamba baada ya kufanya mambo hayo, hawa watu wawiliwawili(me na ke) walijikuta wamezama katika hisia kali za mapenzi ghafla!!
na siku chache baadae , wawili kati yao walifunga ndoa.
na siku chache baadae , wawili kati yao walifunga ndoa.
NA MAMBO HAYO NI:
- -Tafuta mtu mgeni kabisa katika maisha yako
- -Kila mmoja amsimulie kifupi historia ya maisha yake kwa muda wa nusu saa
- -Kisha tizamaneni machoni bila kuongea kwa muda wa dakika 4
Unajua ni kwanini inatokea “unamzimikia” mtu na kujitoa kwa ajili yake kwa chochote!!Twende pamoja:
Hali hii inaendeshwa na kemikali mbalimbali katika ubongo zisizoweza kuzuilika(homoni/hormones).Hua tunafikiria kuwa hua tunachagua wapenzi kwa maamuzi yetu lakini kiukweli kemikali hizi zinafanya kazi kubwa sana katika suala hili kama tunavyoenda kuona:-
Wanasaikolojia wanasemaje? Wanasaikolojia wanasema inachukua kuanzia sekunde 90 hadi dakika 4 kuamua kama “umemzimikia” mtu fulani lakini utafiti unaonesha kuwa hicho kitu kina nafasi ndogo sana na kuongeza kuwa kuvutiwa hadi kufikia kumzimikia mtu kunatokana na:-
- 55%mvuto wa muonekano na umbile lake.
- 38%Sauti anayoitumia wakati mkiwasiliana.
- 7% tu ndio nafasi ya muda kama wanavosema wanasaikolojia.
KARIBU TUENDELEE…
HATUA 3 KATIKA MAPENZI
Helen fisher wa chuo kikuu cha Rotgers alipendekeza hatua tatu ambazo hupitiwa na watu katika mapenzi, nazo ni Anasa, Mvuto na Muunganiko/Mshikamano na kila moja inaendeshwa na homoni mbalimbali kama inavoelezwa;
HATUA 1: ANASA
Hii ndio hatua ya kwanza kabisa kuelekea katika kuzama katika mapenzi,inayochangiwa na homoni ziitwazo testosterone na oestrogen ,kwa wanaume na wanawake. Inamfanya mtu ajisikie hamu ya kufanya ngono.
HATUA 2: MVUTO
Katika hatua hii ndipo unapojiskia kuzama katika mapenzi na mtu fulani hata kabla hamjaongea na kisayansi inaonekana kwamba hali hii inachangiwa na “neurotransmitters” (kemikali zinazotumika katika ubongo kuvusha taarifa kutoka neva moja hadi nyingine) ambazo ni za aina tatu ambazo ni adrenaline, dopamine, na serotonin. Ambazo hufanya yafuatayo:-
Adrenaline: Mwanzoni mtu anapozama katika mapenzi, kiwango cha adrenaline na cortisol huongezeka katika damu , hii humfanya mtu hata kama alikuwa kakasirika awe mchangamfu na mcheshi mara tu anapokutana na mpenzi mpya, ndipo mtu anapoanza kutokwa na kijasho chembamba,mapigo ya moyo huongezeka pia. (Adrenaline pia ndio homoni inayomfanya mtu apate nguvu ghafla anapokutana na hatari inayomfanya hata akwee mti wenye miba bila hata kuhisi maumivu)
Dopamine: Kemikali hii kutoka katika ubongo humfanya mtu awe kama mtumiaji wa mihadarati aina ya cocain. Helen Arthur alifanya uchunguzi wa ubongo kwa watu ambao ni wapya na wamezama katika mapenzi na akagundua kuwa wana kiwango kikubwa cha dopamine. Dopamine humfanya mtu awe na msisimko wa burudani wa hali ya juu, kujihisi ana nguvu nyingi, asiwe na hamu ya kula wala kulala akiwa na mpenzi wake, na kumkosa mpenzi hata kwa muda kidogo humfanya mtu ahisi kama ana “arosto”
(kama umewahi kuwa katika penzi zito unaweza kulithibitisha hili katika comment)
Serotonin Na hatimaye serotonin ,ni kemikali muhimu sana kwa wapenzi, hii inamfanya mtu awe anamfikiria mpenzi wake mpya kila wakati, hawezi akakaa muda mchache bila kumtumia sms au hata kumpigia simu walau asikie sauti yake.Katika hatua hii ndipo watu huwasikiliza zaidi,kuwajali sana na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya wapenzi wao kuliko hata wazazi wao na ndugu wengine ambao wanaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko hata huyo mpenzi wake.
UNAJUA KIPI KINAFUATA KATIKA HATUA YA 3?! ENDELEA…
HATUA 3:MUNGANIKO/MSHIKAMANO
Hapa wapenzi wanakuwa na bond inayowawezesha kushikamana kwa muda mrefu hata kufikia uamuzi wa kupata na kukuza watoto.Kisayansi hali hii inaonekana kuchangiwa na homoni mbili ambazo ni oxytosin na vasopressin. kivipi??
Oxytosine: Hii ni homoni yenye nguvu ambayo hutolewa na wanawake na wanaume wakati wanapofikia kilele wakati wanafanya ngono.hii huzidisha zaidi hali ya kujiskia karibu zaidi na mtu baada ya kufanya nae mapenzi,kadiri mnavofanya mapenzi zaidi ndipo mahusiano yenu yanapokuwa na nguvu zaidi. Oxytosin pia ndio homoni inayozidisha mapenzi ya mama kwa mtoto,na hutolewa wakati wa kuzaliwa na ndio humfanya mama atoe maziwa pale anapomuona na hata anaposikia sauti ya mtoto wake mchanga.
Diane Witt professor kutoka New York alionesha kwamba ukikwamisha utoaji wa kawaida wa homoni hii kwa kondoo na panya hua wana wakataa watoto wao. Na kinyume chake, alipoiweka kwa majike ya panya ambayo bado hayajapandwa, yalianza kujipendekeza kwa watoto wa panya wengine na kuwachukulia kama watoto wao. Kwa hiyo, homoni hii huzidisha upendo hata kama haukuwepo.
Vasopressin:–
Hii pia ni muhimu, nayo pia hutolewa baada ya kufanya tendo la ngono, ambayo kwa jina lingine inaitwa “Anti-diuretic homoni”ambayo mara nyingi husaidia kusawazisha concentration ya chumvi na maji katika damu.Walipoifanyia utafiti kwa wanyama iligundulika kuwa wakiondolewa homoni hii huachana na kutowajali wapenzi wao.
Kwa hiyo usije ukashangaa mtu akazama katika mapenzi na akashindwa kufanya vitu vya msingi na kuishia kutumia muda wake na mali zake kwa mpenzi wake.
Kumbuka “Elimu ni Bahari”, Share na wenzako katika Facebook,whatsapp na linkedin waweze kusoma .
Pia tuandilie maoni yako eneo la COMMENT.
K A R I B U T E N A
No comments