WAPENZI;Kwa Nini Ukiwa Kwenye Mahusiano Huna Uhakika Wa Kuwa Na Furaha
Miaka ya leo watu walio single ni wengi kuliko ambao wameolewa, Sababu iko wazi Ni kukosekana kwa taarifa kamili kuhusu mahusiano. watu wameruka maandiko, Hawajafundishwa au wamesahau .
Kuna mambo mengi siku hizi , Sasa , utakuta mtu anatafuta mtu wa kumpenda, Anatafuta mtu mwenye hamu, mwenye nia. Upendo huo utakuwa kirafiki, wa kuaminika na utakuwa upendo wa kweli?
Fikra za mwanadamu zinahitaji kuwa na upendo usio na sababu, wa kimapenzi na sex iwe ya kufurahisha muda wote kwa mtu mmoja. hafikirii upande mwingine, kujiwazia nafsi yake tu , kwamba apate mtu wa kumpenda. Anatafuta kitu asichokuwa nacho. Hana Upendo ndani yake. Ana uhitaji.
Tunatazama mahusiano ya kimapenzi kwa hali ya juu. Kwa matokeo ambayo sio rahisi mtu kujicommit, Bado watu wengi wanafikiria kwamba , maisha yao hayawezi kuwa kamili wasipokutana na soulmate wake au other half.
Lakini bado ni kitu cha kutoeleweka kwa walio wengi, hawana furaha ndani ya ndoa zao. Ukichunguza huko kabla ya kuolewa alikuwa mtu mwenye furaha.
Sayansi ya Kuwa Single Na Mwenye Furaha.
Tofauti ya furaha ya kuwa Single na kuwepo kwenye mahusiano hutaweza kuielewa mpaka hapo utakapo pitia kwenye mahusiano ambayo hayakuwa mazuri.
Hawa ni wanasayansi wanasema. Lakini kwa mawazo yangu mimi , Kuwa single huwezi kupata furaha kamili unayohitaji. Hata kama utaishi na familia, ndugu na marafiki. hivyo ni vipindi vifupi sana . Muda mwingi utakuwa mpweke katika hali fulani katika maisha yako.
Single ni ngumu . Naongea kutokana na uzoefu wangu. Lakini kama utamjua Mungu , Ukaamua kumtumikia Mungu full time, Utaenjoy usingle wako. Tena basi ni bora hata uwe ulishaolewa au kuoa na kuachana , lakini Kuamua kukaa Single wakati hata hujawahi kuolewa na kuona uzuri na ubaya wa ndani ya mahusiano, Usijidanganye. Utatafuta magonjwa yasio na majina.
Kitu Gani cha Kufanya Endapo Wewe Uko Single.
Anza sasa hivi kuipenda nafsi yako, Anza sasa hivi kujijali, kujithamini, Kujikubali , Kujiheshimu. Kumpenda Mungu Kwa Moyo wako wote, kwa akili zako zote. kwa roho yako yote. Na Umpende jirani yako kama nafsi yako. Huu ndio ufunguo ambao utakufungulia amani yako, furaha yako. Hutakuwa na stress, hutakuwa na woga, mashaka wala wasiwasi.
Ufunguo mwingine ni kutafuta ujasiri wa kuchukua hatua moja nyuma ili kuangalia mahusiano uliokuwa nayo , kwa nini hayakufanikiwa. Halafu jifunze kutokana na hayo na Ufungue Moyo upya wa kupenda.
Mwanaume kwa mwanamke ni lazima awe ni mtu ambaye amejaa masaa yake 24. mkichanganya masaa yenu , yanakuwa 48. Hapo mtaweza kufungua kampuni kubwa na kuishi kwa amani, kwa sababu kila mmoja amejaa masaa yake 24. Anajipenda, anajijali, anajiheshimu, Anaipenda nafsi yake, anampenda jirani yake ,anampenda Mungu, Anafanya kazi anayoipenda, kazi amabayo hatoki jasho. anafanya anachokipenda, na anapenda kitu anachokifanya. .
Ndio, Talaka Inaweza ikakufanya wewe uwe na furaha au Huzuni na kupata maumivu makali.
Kitu hiki kinatokea kwa sababu ya watu kutokuelewa. Niulize swali, Hivi , kama ukiipenda nafsi yako, ukampenda na jirani yako, halafu ukampenda Mungu, Unaweza kumuumiza jirani kweli? Utaweza kumfanyia ubaya? Hata kama ndio ulikosea, kwa nini usiingie kwenye Toba ili Mambo yakae vizuri. Kwa nini usijitahidi kusamehe , Jilazimishe kuingiza Upendo ndani yako kwanza. Unafikiri kama kila mtu angekuwa anajitahidi kuingiza Upendo ndani yake kungekuwa na tatizo la Talaka? HAKUNA.
Kama mtu akimpenda Mungu, mtu huyo anaipenda nafsi yake na anampenda jirani yake. Agizo kuu la Mungu ni Upendo. Upendo hufunuka wingi wa dhambi. Kukiwepo Upendo hakuna talaka, hakuna upweke. Hakuna magonjwa.
Kosa kubwa ambalo wanaume wanalifanya siku hizi, ni kukimbilia kuoa kwa sababu tu ya mwili kuwaka tamaa, Bado hana kazi , hana nyumba, maisha hayajakaa sawa, anaoa kama fasheni. Wanawake kuogopa umri. Eti anachelewa. Lakini hata mimi nilifikiria hivyo mwanzoni. lakini kwangu mimi nilijitamkia mambo ambayo nayaishi mpaka sasa. Kwa hio kuwa makini katika kutamka kwako .mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi.
Sitaki kupunguza kitu, jinsi gani mtu anapata maumivu anapokuwa ameachwa, hasa kama ulikuwa unampenda mtu huyo kupita kiasi chako. upo ugumu mkubwa wa kutafuta furaha, halafu uwe na afya na uishi mwenyewe . Ni matatizo. hisia huja na kuondoka, ni sawa. lakini ni vizuri ukijifunza kujikubali ili uweze kuwakubali wengine ambao wanakuja kwako, ni bora zaidi kuliko kuteseka na upweke.
No comments