CHOMBEZO MWANAMKE JIKUBALI VILE ULIVYO!!


Kuna kasumba ambayo imekuwa ikiwasumbua sana wanawake na wasichana, mahali pengi duniani... kwa kupenda kuwa na makalio makubwa na wakidhani wanaume wanapenda makalio makubwa, imefikia wakati wanawake wanajibinua na wengine wanajipindisha utafikiri ni gari iliyokata center bolt yote hiyo ni kutafuta shape ya mbinuko! Mtakuja kuvunja viuno bure!
Mbaya zaidi ni wale walioamua hata kununua dawa na vifaa vya kuongeza makalio. Napenda kusema kuwa kua kama makalio yangekuwa dili basi wanawake woote wenye makalio wangeolewa. mbona kuna wasichana wenye mbalazo kabisa (flat butts) lakini wameolewa. Mtapata madhara kwa vitu ambavyo havina hata msingi, mjifunze tu kuwa na tabia nzuri kila mwanaume ana kitu anachokipenda kwa mwanamke. na si kwamba kila mwanaume anapenda kitu kilekile na isitoshe mtu kushangaa ndo kwamba anapenda kumiliki ni sawa na ng'ombe wa maonyesho watu wengi huenda kumuangalia kwa fahari ya acho na baada ya hapo wanampotezea.
Jiamini wewe mwanadada na ujikubali vile ulivyo acha kuwa mcharuko!!

No comments