Tiba Sahihi Ya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul ndugu mpenzi msomaji katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote,
Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa na Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake,
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuna sababu zaidi ya 250 zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume,Mtu anaweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo
MAANA YA NGUVU ZA KIUME
Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo la lenyewe.
Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?
Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.
Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.
Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayo pubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.
Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?
Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.
Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:
1. Kukosa hamu ya mapenzi;
2. Uume kusimama kwa uregevu;
3. Kuwahi kufika kileleni;
4. Kuchelewa sana kufika kileleni ( kushindwa kufika kileleni kabisa);
5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa;
6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo;
7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji;
8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;
Mpendwa msomaji, ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.
Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wakadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.
Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezidume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!
Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.
Lakini nini kinachopelekea viungo hivyo vishindwe kufanya kazi vizuri?
Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baaadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation); kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kuleva; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.
Sababu zingine za kupungua nguvu za kiume ni kutokunywa maji ya kutosha, tatizo la kufunga choo hasa pale unapotumia nguvu nyingi kusukuma choo; kutofanya mazoezi; ukosefu wa kumbukumbu; uzito mkubwa/unene mkubwa; kitambi; kuvimba kwa tezidume (Benign Prostate Hyperplasia).
Sababu zingine ni saratani ya tezi dume (Prostate cancer), matibabu ya mionzi ya tezidume na upasuaji, ugonjwa unaoathiri vitendo na shughuli za mwili kama vile mwondoko na balansi (multiple sclerosis), ugonjwa ambao hudhuru mawasiliano ya ubongo na miondoko ikiwa ni pamoja na kutembea, kuongea na kuandika (parkinson’s disease), vyakula vya mafuta, vyakula vilivyowekewa homoni bandia za kike n.k.
Sababu zingine ni maumivu ya mgongo/kiuno; baadhi ya madawa ya kemikali (madawa ya hospitali); kiharusi (stroke); upungufu katika utendaji wa kazi za gonadi (hypogonadism); uzalishaji mwingi wa homoni ya thyroid.
Sababu zingine ni kutozalishwa kwa homoni ya thyroid ya kutosha; ugonjwa unaoathiri uzalishaji wa homoni ya cortisol (cushing’s syndrome); ugonjwa wa kupinda uume (peyronie’s disease); kukakamaa kwa mishipa ya damu (atherosclerosis); orodha ni ndefu sana, ni zaidi ya 200.
Hivyo mwanaume anapopungua nguvu za kiume, ina maana kuna ugonjwa ndani ya mwili wake, au unaweza kuwa huo ugonjwa umeshadhihirika (umeshatokeza) kwa nje, au huo uko ndani ya mwili unamla na kummaliza kimyakimya kama yalivyo baadhi ya magonjwa ambapo baadaye hulipuka. Hii ndiyo maana kitaalamu tunasema kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Unapopungua nguvu za kiume hiyo ni KENGELE YA TAHADHARI kwamba ndani ya mwili wako kuna kitu hakifanyi kazi vyema. Hivyo, unaambiwa kuchukua TAHADHARI kabla ya HATARI!
KOSA KUBWA WANALOFANYA WANAUME WENGI!
Wanaume wengi wanapopungukiwa nguvu za kiume hukimbilia kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume, na siyo kutibu. Hili ni KOSA KUBWA sana!
Ni kosa kubwa kukurupuka kubugia dawa za nguvu za kiume bila kujua chanzo cha tatizo na bila kujua hiyo dawa inakwenda kutibu tatizo gani. Kwa njia hiyo, utamaliza miaka hata zaidi ya 100 na hata miaka elfu moja na hautapona!
Upungufu wa nguvu za kiume lazima utibiwe kuanzia chanzo cha tatizo; kwa maana ya kwamba mzizi wa tatizo sharti ung'olewe kwanza! Mathalani, kama tatizo ni la homoni ijulikane kwanza; kama ni tatizo la tezi ijulikane kwanza, kisha matibabu sahihi yaelekezwe katika maeneo hayo. Hayo ndiyo matibabu, na si vinginevyo. Angalia mwenyewe, upungufu wa nguvu za kiume unaweza kutokana na kisukari kwa mwanaume huyu, au shinikizo la damu la kupanda (HIGH BLOOD PRESSURE) kwa mwanaume yule; au shida ya tezidume kwa mwanaume mwingine au shida ya kihomoni (HORMONAL IMBALANCE) kwa wanaume wengine, basi vipi iingie akilini kwamba wote hao watatibiwa na dawa aina moja? Watu wengi wengi wameelewa kimakosa sana ndiyo maana hata matibabu yamekuwa ni tatizo kubwa sana.
Nani anaweza kutibu nguvu za kiume?
Kuna watu wengi sana hivi leo wanaodai kutibu nguvu za kiume. Ukweli wa mambo ni kwamba siyo kweli! Ni watu wachache sana wana uwezo wa kutibu tatizo la kuishiwa nguvu za kiume. Utakuta mtu anatangaza dawa ya aina moja kuwatibu watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume. Tabia hii pia imejengeka kwa baadhi ya watu, hupiga simu na kuuliza moja kwa moja, "Daktari, dawa za nguvu za kiume ni shilingi ngapi?"
Kila mwanamume ana sababu na chanzo chake cha kupungua nguvu za kiume. Kama wanaume 100 waliopungukiwa nguvu za kiume watajipanga mstari, kila mmoja atakuwa na sababu yake na chanzo chake cha kupungukiwa nguvu za kiume tofauti kabisa na mwingine.
Hii humaanisha kila mgonjwa atakuwa na dawa yake ya kipekee kabisa tofauti na mwingine. Sasa itashangaza kuona huyu kapungukiwa nguvu za kiume kutokana na mishipa ya ateri kutofanya kazi vizuri, na yule kapungukiwa nguvu kutokana na kuvimba kwa tezidume,Halafu wote wapate dawa aina moja! Hiki ndicho kinachofanyika na watu wengi wamepoteza pesa na muda kwa matibabu yasiyokuwa na maana.
Yahitajika daktari mtaalamu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo, ndiye anayeweza kutibu tatizo la nguvu za kiume. Yaani, daktari ambaye anajua vizuri ndani na nje utendaji wa figo, ini, moyo n.k; awe ni daktari wa tiba asilia au daktari wa tibakemikali (yaani daktari wa hospitali) siyo kila mtu tu au kila daktari. Hata kama utakwenda kwenye hospitali kubwa yoyote duniani unayoijua, na ukagonga hodi katika chumba cha daktari, ukamwambia, "Nina tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume," atakurifaa kwa daktari maalumu aliyebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na mfumo wa mkojo. Hata kwa madaktari wa tiba asilia, hali ni hivyo hivyo, lazima ukutane na ambaye amebobea katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
Kwa sababu unapotibu nguvu za kiume unakuwa unatibu viungo vya mwili kwa ujumla. Daktari aliye mtaalamu anakuwa ana uwezo wa kutambua tatizo la kiungo kilichokorofisha mwilini kutokana na kumhoji mgonjwa; na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kujiridhisha kwa vipimo.
LISHE MUHIMU KUREJESHA NGUVU ZA KIUME
wakati mwingine mwanamme hupatwa na tatzo la Nguvu Za Kiume kutokana na kukosa madini lishe muhimu yanayohitajika mwilini mwake.
Naam tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.
Antioxidant Nutrients
Upungufu wa vitamin E, vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa (sperm motility). Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa (International Units - IU) 100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza kumzalisha mwanamke (infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba mwanamke. Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye shahawa (sperm count) na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Tafiti pia zimeonyesha kwamba selenium husaidia uogeleaji wa shahawa.
Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA) ya vitamin C ni miligramu 90. Mwanaume anayevuta sigara anahitaji miligramu 125. Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits), cantaloupe, kiwi, maembe, strawberries, broccoli, cauliflower, pilipili nyekundu na juisi ya nyanya. Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source) na 22 (synthetic). Vyakula muhimu ni pamoja na ngano, karanga na jamii zake, mafuta ya mimea, mbegu zisizokobolewa (whole grains). Selenium RDA ni 15 micrograms. Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood, kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga, vitunguu swaumu.
Vitamin B12
Upungufu wa vitamin B12 hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility. Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa zake, mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).
Zinc
Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa. Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc. Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi kidogo cha homoni za kiume (low testosterone levels). Wanaume wenye shida hiyo wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba. RDA ya zinc ni miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8). Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza, dark turkey meat, lentils, ricotta cheese, tofu, yogurt, spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya. Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.
L-carnitine
Husaidia kuongeza sperm count. Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye nyama na maziwa
NOTED;KABLA YA MATUMIZI YA DAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NI VYEMA UKAWASILIANA NA DAKTARI WAKO WA KARIBU ILI KUPATA USHAURI ZAIDI
Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini
No comments