JIFUNZE Mambo 10 Ambayo Nimejifunza Kuhusu Upendo

young-couple-in-bed1 Mambo 10 Ambayo Nimejifunza Kuhusu Upendo
Nimekuwepo katika mahusiano ya muda mrefu , na pia mahusiano ya muda mfupi kwa zaidi ya miaka kumi.
Nimekutana na mahusiano mazuri na mabaya. ya kuridhisha na ya kutoridhisha.Nimekataliwa, nimeshangazwa kwenye kichwa changu kwa kiasi kikubwa.Kupitia safari yangu nimekutana na baadhi ya mafunuo.
1.Upendo sio Uwanja wa Vita.Ni Kichwa chako 
Kila kitu kipo kwenye masikio yetu ndiko tunakopatia uzoefu.Ni mawazo yetu, kujiunganisha kwetu, kuelewa kwetu na imani yetu wenyewe. kila kitu kinatokana na historia .
Uharibifu upo, lakini unatokea wapi, sio kwenye upendo wetu. unatoka ndani yetu. Uharibifu hautoki kwenye upendo. Sumu haitoki kwenye upendo. inatoka kwenye kukosekana kwa uelewa. Wivu hautoki kwenye upendo. Unatoka kwenye kukosa usalama.Hisia badala ya ukweli hautoki kwenye upendo, unatoka kwenye kutofahamu.Upendo  sio uwanja wa vita,ni kichwa chako. Kuwa makini na mawazo yako, na maswali yako.
2.Hakuna mtu Sahihi
Kila mtu anataka mwenza sahihi. lakini kama ndio lengo lako , utacheza mchezo huo  siku zote. hakuna mtu sahihi, Lazima ufahamu hili. lakini watu wamekuwa wakiendelea kutafuta mtu sahihi. hii inaleta kuhukumu na kulaumu watu bila kosa. Acha kufikiri kupata sahihi.kwani hio sahihi inaonekanaje, kuna lable au  maelezo yoyote?  Utaendelea kuvua samaki kwenye swiming pool ndogo ya plastic.
Ni wakati wa kuacha kutafuta maelezo ya sahihi. hakuna badiliko lolote la sahihi. Ni bora kupata ambacho sio sahihi, ukakisahihishe ndani. futa kabisa sahihi ndani ya akili yako. Unatafuta mtu ambaye hujawahi kuvutiwa naye, kitu kipya, fresh au tofauti. kwa sababu katika mlango huo kuna kujifunza mafunuo mapya. kitu kinachohusu mapenzi, kitu kipya ambacho hakirudiwi.
3.Uchumba Unaweza kuwa Mzuri.
Wakati mwingine unaweza ukawa mbaya, lakini ukawa ni mzuri. ni kweli, inawezekana , nimekuwepo huko ilinitokea.  kosa kubwa ambalo watu hulifanya ni kuweka matarajio makubwa , na baadae kutokutana nayo.  matarajio ya jinsi ambavyo atafanya kitandani,  atakavyofurahia, atakavyopenda mahusiano.
Unatakiwa uwe na matarajio ya kukutana na mtu mpya, kujua historia mpya, kujifunza kutoka kwa mtu mpya,  kutaka kumfahamu  mtu, kusikiliza na kupata uzoefu.
4.Kama huna uhakika na mtu usiwekeze kwake.
Mahusiano ni magumu.Kama utamtaka mtu awe na wewe kwa kulazimisha, unafikiri itakuaje? kama mtu hana uhakika  na wewe kwa nini utake kuwa naye kwa lazima. Kwa sababu hio tunamaanisha kuwa tunastahili, tunataka, tunathamini. lakini hatufikirii mahusiano hayo yataonekanaje. nitakuambia. yatakuwa ni ya muda mfupi.  Nimejifunza kutolazimisha mtu kwa sababu haitafanya kazi. utakuwa unaboreka muda wote.
5.Upendo ni kama kumenya kitunguu maji sio kutafuna apple
Ganda la juu sio upendo ni kifuniko. ni ngozi, ni tamaa au matamanio.mihemiko. Upendo hautokei mpaka hapo utakapo menya ngozi ya juu. ni pale utakapoona kila upande  na kukubali na kukumbatia hicho na kuchagua kupenda kilivyo.
Wengi hutazama juu, unafahamu hisia. lakini hisia  peke yake hazijengi afya, hazidumu, hazileti maana kamili ya mahusiano. Lakini kuna kitu cha zaidi. na cha kugundua zaidi, ambacho hakijapatikana. Ni zaidi ya kukutanisha macho  mahali.
Upendo ni kumenya kitunguu pamoja, kupata uzoefu pamoja, kujifunza kwenye changamoto pamoja, kushikana mikono, kujifunza, kukua pamoja,  kuchongana  pamoja safarini.
6.Kama mtu atataka kuwa na wewe utajua 
Nimejifunza kama mtu anataka kuwepo na wewe utafahamu. kwa sababu atakuambia wazi kabisa kuwa anataka kuwa na wewe. hata kama bado hajawa tayari katika mambo yake mengi , lakini atakuambia wazi. Ingawa atakuwa na woga. hakuna mtu asiyeogopa, lakini maamuzi hufanyika . Na hasa kama kweli anakutaka utajua. Kwa kuwa watajitahidi kutumia nguvu fulani, watajaribu. watawasiliana, hawatakimbia wala kujificha.
7.Hakuna Mtu ambaye huwa Tayari Kwa Ajili Ya Mahusiano.
Mahusiano ni kama kupata mtoto. wakati mwingine unaweza kupata mtoto bila ya kujiandaa. utafanya na kujikuta mabadiliko yametokea. mambo hutokea unapojisikia kufanya hivyo. kitu kinachofanya au kusaidia kujiandaa ni kutokana na msaada wa vitabu, makala ya mahusiano,  seminars. hivi vitu ndio vinakufanya uwe hivyo. lakini ukweli ni kwamba hakuna muda maalumu . hujui ni lini utakutana na mtu amabye atakuvuta moyo wako , mtu wa kukuvua soksi zako. huenda ni mtu ambaye unamfahamu tayari,  ambaye umekuwa ukimuona tofauti. nilichokigundua ni hiki. ni wakati unatarajia au kutotarajia.unapokuwa tayari au hujawa tayari.
Hakuna kitu cha utayari. kwa sababu kila mtu anakosea, tunabadilika, tunaanguka, tunainuka tena. kwa hio kama umekutana na hali hio usihofu. penda kwa kadri unavyoweza.
8.Kumbatia Upendo Ulionao
Kuna mtu aliniambia nikumbatie upendo kwa mikono yote miwili na kwa moyo ulio wazi. Watu wengi hunyakua upendo, na upendo huo huondoka mikononi mwao. kwa sababu nyuma yake huwa kuna hukumu. Wengine hufikiria kunyakua upendo ni kupenda kwa nguvu. lakini ni kinyume chake. Fikiria upendo kama unavyojaribu kumlisha ndege, halafu unamkimbiza, atakimbia, lakini kama ukishikilia chakula mkononi mwako , ndege atakuja na kula , ataanza kukuamini, utaona kila mara anakuja kwako. Upendo ni kushikilia , kukua nao na kuaminiana.
Shikilia Upendo , Usinyakue  upendo.
9.Unaweza kupenda kwa ugumu
Ugumu unaonekanaje. Kupenda kwa nguvu zaidi sio kuonyesha kumjali mtu zaidi. inaweza ikawa na maana ya kumpa mtu nafasi. Inaweza ni katika kuangalia afya yako mwenyewe, Inaweza ikawa ni katika kujikubali. Inaweza ikawa ni katika kujishughulikia mwenyewe, kuachilia, au kutokukata tamaa.
Jiulize mwenyewe, upendo huu unaonekanaje kwako. Sehemu nzuri ya kutazama ni hii, unatoa au unapokea?  Wengi wanamini wanatoa lakini kumbe wanachukua. Kama unatumia upendo ili kupata furaha mwenyewe, unachukua. Kama unatumia upendo kutawala mtu , unachukua, kama unatumia upendo ili kuziba pengo lako, unachukua.  Kutoa ni kushirikiana na mwenzako, kutoa ni kuja pamoja kama mtu mmoja. kumkubali mtu jinsi alivyo na kuwapongeza  na kusikiliza .
10 Usiache Kuamini.
Wote tumekataliwa, wote tumeumizwa kwa njia moja au nyingine. wote tumepita katika mambo ambayo hatukutarajia. mambo ambayo hayakuwa na maana, tumesalitiwa, tumedanganywa na kuachwa peke yetu. Kutokana na hayo tumejikuta hatuwezi kuamini tena. upendo umekuwa mbali nasi.
Lakini nakuambia kuwa, tulichokiamini kinaweza kuwa ni usukani tunakoelekea. hii sio tu upendo. ni katika kila kitu. Imani yetu inatokana na uzoefu wetu. kwa hio kama tutaamini upendo haupo, hautakuja. lakini tukiamini kuwa kuna upendo, tutauona.
Kwa hio ni vizuri kuendelea kuamini, kwa kila pumzi ya uhai wetu kuwa upendo upo. kwa sababu hata kama hutaamini bado upendo upo tu.
Maisha yanahusiana na Upendo.Na upendo ndio unaotufundisha  jinsi ya kuishi.

No comments